HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 3 October 2018

Bank ya CBA yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kusherehekea na wateja wake

Benki ya CBA yajivunia mafanikio waliyopata baada ya kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi makamu Mkurugenzi,Julius Konyani amesema kuwa benki iyo ndani ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania,himeweza kupata mafanikio kupitia wateja wao.

Aliendelea kudai kuwa ndani ya miaka hiyo kumi benki iyo imeweza kuwa na wateja wengi wakiwemo wafanya biashara wakubwa na wadogo na kudai kuwa benki hiyo inatoa mikopo kwa wateja wao.

"Benki yetu ndani ya miaka 10 imeweza kutoa mikopo kwenye makampuni na wafanya bishara ambao ni wateja wao"alisema makamu mkurugenzi

Naye mteja wa benki iyo ambaye ni mfanyabiashara,Isack Lazaro alisema kuwa kupitia benki ya CBA ameweza kupata mafanikio makubwa hasa katika biashara zake.

"Nilijiunga na benki hii muda mrefu sana,nadhani mimi ni mmoja wapo wa  wateja wa mwanzoni kujiunga na benki ya CBA tangu ilipoanzishwa Tanzania"alisema Isack

Mteja huyo aliendelea kudai kuwa kupitia biashara zake ameweza kupata mikopo katika benki hiyo kwaajili ya kuweza kuendesha biashara zake kwa kuongezea mtaji.

Naye mteja mwingine wa benki hiyo,Enock Mwakipesile alidai kuwa tangu ajiunge na CBA benki ameweza kunufaika nayo katika mambo mengi hasa katika biashara zake.

"Tangu nijiunge na CBA nimeweza kunufaika nayo katika mambo mengi hasa kibiashara,nimeweza kuendesha vizuri biashara zangu na ninapohitaji mkopo wamekuwa wakinipa pamoja na kunishauli mambo ya kibiashara"alisema mteja
wa benki hiyo Enock

Hata ivyo benki iyo imekuwa ikitoa semina mbalimbali kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa katika sehemu mbalimbali nchini.
 Kaimu Mkurugenzi wa benki ya CBA Tanzania,Julius Konyani (kulia) akikata keki pamoja na wateja wa benki jiyo,Isack Lazaro (kushoto) na Enock Mwakipesile,katika mwendelezo wa kuathimisha miaka kumi ya kuanzishwa kwa benki iyo nchini Tanzania,waliosimama nyuma ni wafanyakazi wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa benki ya CBA Tanzania wakiwa katika picha ya moja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad