HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 25, 2018

WAZIRI WA NISHATI AELEZA NAMNA AMBAVYO SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI MADHUBUTI SEKTA YA MAFUTA NA GESI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Nishati Dk. Medradrd Kaleman amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha Watanzania wanakuwa wanafuika namba moja katika miradi mikubwa inayoendelea nchini.

Pia amesema katika kuhakikisha sekta ya nishati na gesi inawanufaika Watanzania wa makundi yote Serikali imeweka sera na mikakati madhubuti itakayosimamia vema maslahi ya nchi.


Waziri Kalemani amesema leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzungumza kwenye Kongamano la Pili la mafuta na gesi ambapo wadau zaidi 300 kutoka mataifa 75 duniani wameshiriki na kutoa maoni yao.


Akifafanua zaidi kuhusu namna ambavyo Serikali imejiandaa katika kuhakikisha sekta ya mafuta na gesi Waziri Kaleman amesema kikubwa ambacho wanahamasisha ni wananchi kushiriki katika sekta hizo na hasa miradi mikubwa inayoendelea ili waweze kunufaika.


“Tumewaambia wawekazaji wote ambao wamefika hapa na wale ambao wanayo miradi mikubwa wanayoendelea kuitekeleza kuhakikisha wananchi wetu wanashirikishwa na kunuifaka.


“Kuna kazi ambazo hazina sababu ya kufanywa na watu wa nje.Tunafahamu Watanzania wamesoma kwa viwango tofauti lakini kila mmoja lazima ashiriki kwa nafasi yake na anufaike na uwepo wa miradi inayoendelea nchini,”amesema Waziri Kalemani.


Amefafanua katika kushiriki huko ni matarajia ya Serikali kuwa kampuni ambazo zinahusika na chakula basi vitauza chakula, kampuni za kisheria basi nazo zitatoa ushauri wa kisheria na kwamba kila kampuni, kikundi au mtu mmoja mmoja lazima ashiriki na tayari Serikali imeweka mazingira mazuri.


 Pia amezungumzia hisa ya asilimia 25 kwa ajili ya wazawa na kwamba muwekezaji yoyote ambaye anataka kuja kuwekeza nchini katika gesi na mafuta basi lazima asilimia 25 ya uwekezaji iwe ya watanzania.


 Amewahakikisha Watanzania kuwa Serikali imejipanga vema kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinawanufaisha.


Wakati huo huo amesema mkutano huo umedhihirisha namna ambavyo sekta binafsi wanashirikiana na Serikali katika kutoa muelekeo kuhusu sekta hiyo.
Waziri wa Nishati Dk.Medrard  Kalemani akifafanua jambo baada ya kuzungumza leo jijini Dar es Salaam  kwenye Kongamano la Pili la mafuta na gesi ambapo wadau zaidi ya 300 wameshiriki.
Mwaandaji wa Kongamano la pili la gesi na mafuta ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la  Watumiaji Huduma za Mafuta na Gesi(ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar  es Salaam kuhusu ajenda zilizojadiliwa kwenye kongamano hilo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad