HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 17 September 2018

WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bibi Jo Dedeyne ambaye ni  Katibu Mkuu Kiongozi wa Taasisi za  Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia dawa za kulevya na uhalifu (United Nations Office on Drugs na Crime - UNODC)  baada ya kufungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Azungumzia dawa za viwandani zinavyotumika kama dawa za kulevya

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 huku akieleza kuwepo kwa mbinu mpya ambapo dawa za viwandani zimeanza kutumiwa na baadhi ya watu kama sehemu dawa za kulevya.


Hivyo amesema ipo haja ya kuhakikisha kunakuwa na mikakati mipya ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya huku akiomba wakuu wa vyombo vinavyohusika na kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika kuweka mikakati ya kuiabiliana na mbinu mbalimbali ambazo zinatumiwa na wanaofanya biashara hiyo.

Waziri Mkuu amesema hayo leo baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC),ambao unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza ipo haja kwa nchi hizo kuangalia kwa namna gani wanaweza kuweka mikakati ya kukomesha biashara ya dawa za kulevya.
Ameeleza namna ambavyo baada ya kufanikiwa kudhibitiwa kwa dawa za kulevya wapo baadhi ya watu wasiwaaminifu ambao wanachukua dawa zinazotengenezwa viwandani kama sehemu ya dawa za kulevya.


Ametoa mfano wa dawa hizo ni pamoja na dawa za usingizi ."Zipo dawa zinazotengenezwa viwandani watu wasiowaaminifu wanazichukua na kisha kuzibadilishia matumizi kuwa dawa za kulevya,"amesema.

Hivyo amesema lengo la  mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo.

“Ni lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kudhibiti uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika. Hata hivyo ni muhimu kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya," amesema Waziri Mkuu.

Pia ametoa mapendekezo kwa washiriki wa mkutano huo kuangalia uwezekano wa kuwa na sheria moja kwa nchi za Afrika katika kukabiliana na dawa za kulevya.
Ameongeza kwa sasa wanaojihusisha na biashara hiyo wamekuwa wakitumbinu mpya za kusafirisha dawa hizo,hivyo ni vema mkutano huo ukatoka na maazimio ambayo yatasaidia kudhibiti usafirishaji wa dawa hizo.

Ametumia mkutano huo mkutano huo kueleza kuwa Tanzania inaendelea na mikakati ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya ikiwemo uzalishaji wa dawa hizo ikiwemo mirungi na bangi, ambayo inapandwa kwa kuchanganywa na mazao ya chakula.


"Tanzania ni nchi ya kwanza katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha vituo vya utoaji wa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya mwaka 2011. 

" Hadi kufikia mwishoni mwa 2017, jumla vituo sita vya kutolea matibabu vilianzishwa, ambapo zaidi ya waathirika 6,500 wa dawa za kulevya aina ya heroin walijiandikisha na kupatiwa matibabu,"amesema.

Wakati huo huo baadhi ya washiriki wameeleza kwamba kasi ya matumizi ya dawa za kulevya imeshika kasi na ukanda wa Kusini mwa Janga la Sahara limekuwa likitumika kama njia ya kupitisha dawa hizo.

Imeelezwa kwa mwaka jana ukanda huo ukiwamo wa nchi za Afrika Mashariki tani zaidi ya 200 za Cocain zimepitishwa.

Pia imefafanuliwa moja ya changamoto kubwa imetajwa kuwa biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin  zinafanywa zaidi na wanaojihusisha na ugaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad