Na Mwandishi Wetu.
WATAALAM wa Afya kutoka Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya.
Ujio huo wa wataalam 9 umeongozwa na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani, Dkt. Deborah Stith akiwa na wataalamu hao wakiwemo madaktari wa macho, mfumo wa mkojo na meno.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema lengo la ugeni huo ni kuangalia jinsi ambavyo pande hizi mbili zinavyoweza kunufaika kwa kujenga mahusiano katika ufundishaji ,kuboresha huduma pamoja na utafiti.
“Ushirikiano ambao tunautafuta hasa ni katika nyanja ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujuzi madaktari wetu katika sehemu tulizokuwa tunafikiri kutoa huduma ambazo tulikuwa hatutoi awali” Amesema Prof. Museru.
Aidha Dkt. Deborah Stith amesema wako tayari kushirikiana kwa karibu na Muhimbili kwa kubadilishana wataalam kwa manufaa ya jamii.
No comments:
Post a Comment