HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 12 September 2018

WANARIADHA WANANE KUSHIRIKI HALF MARATHON OKTOBA 07, NCHINI UINGEREZA

Tanzania itawakilishwa na wanariadha wanane katika mashindano ya riadha ya nusu marathoni yanayotazamiwa kufanyika Oktoba saba katika Mji wa Cardiff nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Shirikisho la mvchezo wa riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabudai mashindano hayo ya nusu marathoni ni ya kwanza kuandaliwa na Jumuiya ya Madola.

Baadhi ya wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza ya nusu marathoni yaani kilometa 21.

“Ni mashindano ambayo nchi inawakilishwa moja kwa moja, ni sawa na mashindano ya jumuiya ya madola yaliyoandaliwa nchini Australia,” Gidabudai ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya Radio France.

Baadhi ya wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania ni Fabiano Nelson, Sara Ramadhan, Fainuna Abdi na Pascali Mombo.

Hata hivyo Tanzania, itakabiliwa na kibarua pevu kuwania medali katika mashindano hayo, kutokana na uwepo wa wanariadha kutoka mataifa ya Kenya na Afrika Kusini ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.


Credit: RFI, Fredrick Nwaka 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad