HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 7 September 2018

WANAFUNZI WATATU WA IFM WAPATA UFADHILI WA ADA YA MWAKA WA TATU

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Wanafunzi watatu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamepata ufadhili kusoma mwaka wa tatu kwa kulipiwa ada kupitia kampuni ya Bima ya Metropolitan.

Akizungumza wakati wa kupokea hundi ya sh.milioni 4.5 Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Immanuel Muzava amesema kuwa kampuni ya Bima ya Metropolitan kupitia Chama cha Mawakala wa Bima (TIBA) kimefanya jambo la kuigwa katika umuhimu wa kusaidia wanafunzi ambao wana uhitaji wa kuweza kuhitimu masomo yao.

Muzava amesema kuwa sekta ya Bima inakua kwa kasi nchini hivyo lazima kuwepo na watalaam wa kutosha.

Wanafunzi waliopata ufadhili huo Paschalina Msofe,Rhoda Maholy pamoja na Leonard Mahimbo.

Amesema wanafunzi hao walikuwa na changamoto ya kiuchumi ambayo ingewafanya wakwame kuhitimu mwaka wa tatu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar amesema kuwa wanajibu wa kufanya hivyo bila kulazimishwa.

Amesema kuwa watu wakipewa elimu kunaongeza tija kwa serikali katika kuwa na watalaam wataosaidia maendeleo ya uchumi.

Aidha amesema waliofadhiliwa sio wakihitimu wakafanye kazi katika kampuni hiyo bali watafanya sehemu yeyote ikiwa nia kutoa huduma ya bima katika maendeleo ya nchi.

Mmoja wa wanafunzi waliofadhiliwa Paschalina Msofe amesema kuwa kazi yao ni kusoma bidii na kutoa matokeo mazuri kwa kile walichosome katika utoaji wa huduma ya bima nchini.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar akizungumza wakati wa kupokea hundi ya wanafunzi waliofadhiliwa katika chuo hicho.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar akizungumza kuhusiana na kampuni hiyo kufadhili ada kwa wanafunzi.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Immanuel Muzava  akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar kwa ajili ya ada kwa wanafunzi kwa ada ya mwaka wa tatu.
 Mwanafunzi wa IFM Rhoda Maholy akitoa shukurani kwa niaba wanafunzi wenzake kuhusiana msaada kusoma mwaka wa tatu kwa ufadhili.
Wanafunzi wa IFM wakiwa na hundi ya mfano wa ada ya iliyotolewa na Kampuni ya Bima ya Metropolitan.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad