HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 17 September 2018

WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO

 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
 Mkurugenzi Msaidizi upande wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka akielezea lengo na umuhimu wa mafunzo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bw. Paschal Mahinyila akitoa salamu za Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo wa wakuu kwa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
 Mwakilishi kutoka NACTE Bw. Gidion Karuguru akitoa muongozo wa matumizi ya Mtaaka Mpya kwa Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Wakuu wa Vyuo na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakifuatilia mafunzo ya Mtaala mpya kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi nchini  uliopitishwa na NACTE hivi karibuni utakaoanza kutumika kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Picha zote na Kitengo cha Mawasilino WAMJW

Na Mwandishi Wetu Singida
Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi nchini wameaswa kutoa wataalamu wa maendeleo ya Jamii wenye viwango vya juu ili kuendana na ushindani uliopo na katika kufikiamuchumi wa kati na wa viwanda.

Hayo yamesemwa leo Mjini Singida na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni na utakaoanza kutumika kwa mwaka wamasomo 2018/2019 mpaka mwaka 2022/2023.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bw. Golwike amewapongeza wakuu wa vyuo na wakufunzi hao kwa kazi nzuri wanaoendelea kufanya katika kutoa wataalamu wenye viwango katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.

 Ameongeza kuwa wakufunzi hao wanatakiwa kuongeza nguvu katika kutengeneza wataalamu wengi wenye viwango zaidi ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na ushindani katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.

“Tutengeneza wataalamu wenye viwango ili tuendane na mabadiliko hasa kuelekea uchumi wa viwanda” alisisitiza Bw. Golwike

Aidha Mkurugenzi Msaidizi upande wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka akimkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuzindua Mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wakufunzi katika kuwajengea uwezo wa kufundisha na kutoa wataalamu wenye viwango katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jami Monduli Bw. Salimu Mgalla kwa niaba ya wakufunzi wengine ameishukuru wizara kwa kuwakutanisha wakufunzi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi na kuwapitisha katika Mtaala mpya utakaotumika na vyuo hivyo.

“Tunakuahidi kuwa yutakuwa bora katika kutoa wataalamu hata kuliko Taasisi nyingine katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini” alisisitiza Bw. Mgalla

Wakuu wa Vyuo na wakufunzi kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wapo katika mafunzo ya siku kumi ya kupitishwa katika mtaala mpya utakaotumika katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad