HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 19, 2018

Tigo na Clouds Wazindua Msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote kupata vibali kutoka kwa baraza hilo. Tigo Fiesta 2018 inatarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) .

Tamasha la kusisimua zaidi la muziki na utamaduni Afrika Mashariki na Kati, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Lama Lote sasa lipo tayari kukonga mioyo na 100% mziki wa nyumbani katika mikoa 15 ya nchi. Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2018 ni Vibe Kama Lote, ikiashiria burudani maridhawa na ladha ya kumbukumbu zisizofutika zinazoendana na msimu huu nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alibainisha kuwa, msimu wote wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote utashuhudia burudani 100% kutoka kwa wasanii wa kitanzania, kufuatia mafanikio makubwa ya mfumo uliotumika mwaka jana. Shangwe zinatarajiwa kuanza mjini Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 29 Septemba.

‘Muziki ni nguzo muhimu ya kampuni yetu, kwa hiyo Tigo Fiesta 2018 itadumisha asili yake ya kuvumbua na kukuza vipaji vya Kitanzania. Lengo letu kuu ni kukuza tasnia ya muziki na kutoa fursa za ajira kwa vijana na jamii yote kwa ujumla’ William alisema. Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Gardner G. Habash alisema kuwa katika historia yake ya miaka 17, Tigo Fiesta imekuwa jukwaa la kukuza muziki wa nyumbani. ‘Tigo Fiesta inawapa fursa wasanii kuonesha uwezo wao na kuongeza idadi ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Kuna maelfu ya mashabiki wanaohudhuria matamasha yenyewe au kufuatilia matukio kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,’ alisema.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) .

Mbali na kutoa burudani ya uhakika, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote pia itaibua fursa nyingi za kujiongezea kipato kwa wasanii pamoja na wakaazi wa maeneo mbali mbali yatakayoshuhudia shamrashamra za msimu huu.

Pia katika msimu huu wa burudani, Tigo inatoa tiketi za watu mashuhuri (VIP) za kuhudhuria Tigo Fiesta 2018 kwa wateja ambao watanunua vifurushi vya Tigo VIP Pack ambavyo vinawapa wateja huduma bora zaidi za sauti, SMS na data kuanzia TSH 30,000/-. Vile vile, wateja wote wa Tigo pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi kem kem kama vile pesa taslim na simu janja kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta Chemsha Bongo ambapo watatakiwa kujibu maswali yanayohusu Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote.
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es salaam katika uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati). 

‘Wasanii wenyewe pamoja na jamii yote kwa ujumla katika mikoa 15 itakayotembelewa na msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote watapata fursa kubwa za kiuchumi zinazoendana na msimu wenyewe,’ William alisema. Wafanya biashara mbali mbali ikiwemo wamiliki wa hoteli, migawa, kumbi za starehe, mama niitilie, wauzaji wa nguo na wamiliki wa vyombo vya usafiri huongeza kipato kutokana na biashara zao kuchangamka kutokana na idadi kubwa ya wateja wanaohudhuria matamasha ya Tigo Fiesta.

Gardner aliongeza kuwa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote utajumuisha miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad