HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 3, 2018

TAA YATOA MSADA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WABUNGE WANAWAKE KUJENGA VYOO VYA SHULE NCHI NZIMA

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela (wakwanza kulia) akiwaongoza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa chas Julius Nyerere (JNIA) Bw. Paul Rwegasha (watatu kulia) na Afisa Uhusiano Bi. Bahati Mollel (wapili kulia) kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 (5,000,000/=) kwa mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Hafla hiyo ilifanyika usiku wa kuamkia leo Septemba 1, 2018 jijini Dar es Salaam.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge hilo, (TWPG) kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga vyoo salama vya shule nchi nzima kwa mtoto wa Kike kwa kutoa mchango wa kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000).
Katika hafla ya kuchangisha fedha kwa dhumuni hilo, iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela, alikabidhi msaada huo wa fedha kwa mgeni rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa (TWPG), ambaye pia ni Mbunge wa Urambo, Mhe.Margareth S. Sitta, wazo la kutafuta fedha za ujenzi wa vyoo hivyo ni katika jitihada za kuhakikisha wanafunzi wote hususan wa kike, wanafurahia haki yao ya msingi ya kupata elimu katika mazingira rafiki na masafi bila kujali changamoto zinazosababishwa na tofauti zao za kimaumbile.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliwapongeza Wabunge hao kwa hatua hiyo ya kuhakikisha kunakuwepo kwa  mazingira bora shuleni ili kutoa haki sawa ya kupata elimu kwa wanafunzi wote.
“Wazo hili litasaidia sana serikali katika kuhakikisha mazingira ya shule yanaboreshwa ili kutoa nafasi sawa kwa wanafunzi wote wa kike na kiume” alibainisha Spika Ndugai.
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa sana na kitendo hicho na kwamba ameshindwa kuhudhuria hafla hiyo kwa vile bado yuko kwenye msiba wa dada yake huko Chato Mkoani Geita. 
Kwa upande wake, mgeni rasmi Mhe. Anne Makinda aliwapongeza wabunge hao wanawake kwa hatua hiyo ya kuunga mkono juhudi za serikali na kuwataka Wabunge wanaume kuwaunga mkono wenzao katika kufanikisha kampeni hiyo inayolenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.5 zitakazowezesha kujenga vyoo vya shule kwenye majimbo yote 264 nchi nzima.
Taasisi mbalimbali zilichangia kwenye harambee hiyo.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, akizunhgumza.
 Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Margareth S. Sitta, akitoa hotuba yake.
 Mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda, akitoa nasaha zake.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akitoa nasaha zake.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, akifuatilia kilichokuwa kikizungumzwa na viongozi.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akifurahia jambo.
 Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifuatilia hafla hiyo.
 Meza ya wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji nchini.
 Spika Ndugai akiongoza wabunge wengine kusakata rhumba
 Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni msanii wa muziki, Mhe. Martha Mlata akiimba kwenye hafla hiyo.
 Wabunge wa Viti Maalum wakisakata rhumba.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiongozana na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakati wakiingia ukumbini.
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kiwkete akiwa na Mbunge wa jimbo la Segerea, Mhe. Bonner Kalua

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad