HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 6 September 2018

StarTimes yaongeza kasi kupambana na UKIMWI

Kampuni ya StarTimes na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ugonjwa wa UKIMWI UNAIDS, wamekutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ushirikiano wao katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo. Mkutano huo uliopewa jina la “Thamani ya Taarifa kwa njia za kidigitali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI” ulihudhuriwa na Makamu Rais wa StarTimes Group Bi. Guo Ziqi, Mke wa Rais wa Malawi Bi. Gertrude Mutharika na Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Bw. Michel Sidibe.

Katika mkutano huo ambao umefanyika mapema mwanzoni mwa wiki hii jijini Beijing, baadhi ya mambo yaliyoongelewa ni ongezeko la vifo vilivyosababishwa na UKIMWI kwa Vijana hii inatokana na kutofikiwa na taarifa juu ya maambukizi ya VVU/UKIMWI hivyo wanakosa ufahamu juu ya njia sahihi za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huo.
Bw. Michel Sidibe akizungumza katika mkutano huo alisema “Tumejionea mwenendo mzuri katika nchi nyingi lakini changamoto tunayokutana nayo ni kukata tama. Vijana wengi hawana taarifa, hawana ufahamu, hivyo hawajilindi na maambukizi..kwa hiyo taarifa, ufahamu na elimu ni muhimu na ndio maana tunajivunia kufanya kazi na StarTimes katika hili.”
Michel aliongeza, “nataka tu kusema kwamba kupeana taarifa na kueleweshana juu ya UKIMWI ili kuwabadilisha vijana itakuwa ni hatua muhimu sana katika kutokomeza ugonjwa huu”. Pia alisema kwenye nchi nyingi za kiafrika zaidi ya asilimia 70 ya watu wote wana umri wa miaka 35 na hawapati taarifa kuhusu ugonjwa huu. “njia yetu ya kukabiliana nao itabadilisha kila kitu na pengine tutakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya UKIMWI”, aliongeza.
Kwa kupitia teknolojia ya mawasiliano ya intaneti kwenye simu barani Afrika na kwingineko duniani, mawasiliano yatakuwa muhimu zaidi katika mapambano haya.
“Kwa kulitambua hilo, StarTimes tulianzisha huduma ya kupata video za moja kwa moja kwenye simu barani Afrika, StarTimes App ambayo tuliizindua mwezi wa sita, na tayari miezi mitatu baadaye imepakuliwa na watu milioni 8 tunategemea watafikia milioni 15 kufikia mwisho wa mwaka”, aliseama Bi. Guo Ziqi.
Kwa sasa tayari StarTimes wanatoa huduma ya kustream maudhui yanayofahamika kama “Zero Discrimination” ikishirikiana na UNAIDS.
Naye mke wa Rais wa Malawi Bi. Gertrude Mutharika alisema, “Ushirikiano wa StarTimes na UNAIDS katika kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI umekuja kwa wakati sahihi kabisa ambapo Malawi na Afrika kwa ujumla tupo katika mapambano haya muhimu kwa bara letu”.
Viongozi wa Afrika walikuweko jijini Beijing kuhudhuria kongamano la vyama vya Kisiasa vya Africa na kile cha China FOCAC katika kuimarisha uhusiano wa Afrika na nchi ya China.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad