HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 September 2018

RC MAKONDA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA BARABARA KIGAMBONI, AWAHIMIZA TANROAD NA TARURA KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Madaraja inayotekelezwa na Serikali kwenye Wilaya ya Kigamboni ambapo kukamilika kwake kutafanya mji wa kigamboni kuwa wa kisasa zaidi.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na RC Makonda ni ujenzi wa Barabara ya njia sita za magari kuelekea Daraja la Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Kilomita 2 pamoja Mzunguko wa Magari (Round about) yenye ukubwa wa Mita 250 kuelekea Feri Mita 250 kuelekea Kibada ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika October 31 mwaka huu.

Aidha RC Makonda ametembelea ujenzi wa Barabara ya KKKT na mitaro ya maji yenye urefu wa Mita 275, Barabara ya Hospital ya Vijibweni Mita 800 kutoka Kibada,Barabara ya Kijaka-Mwasonga Km 8, Mwasonga-Kibada Km 16 Kimbiji-Pembamnazi, Daraja la Puna eneo la Buyuni na Daraja la Kibugumo Kata ya Gezaulole ambapo miradi hiyo ipo hatua za mwisho kukamilika. 

RC Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo na kuwahimiza TANROAD na TARURA kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waendelee kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema wamejidhatiti kuhakikisha Kigamboni inakuwa na Barabara za Lami, Maji ya kutosha na Umeme kwaajili ya Viwanda, Makazi na Showroom kubwa Africa Mashariki na Kati.
TULIAHIDI NA TUNATEKELEZA.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza leo na waandishi wa habari juu ya kuwahimiza Tanroad na Tarura kukamisha miradi kwa wakati katika wilaya ya Kigamboni.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akisikiloza kero za wananchi wa wilaya ya Kigamboni leo katika ziara ya kukagua miradi ya barabara katika wilaya hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambata na viongizi mbalimbali wakikagua miradi mbalimbali  katika  wilaya  ya Kigamboni.
 Mafundi wakiendelea na kazi.

Muonekano wa maadhi ya madaraja yanayojengwa katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad