HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 9, 2018

PROF KITILA MKUMBO AZINDUA MENEJIMENTI YA DAWASA MPYA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amezindua menejimenti mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASA) itakayokuwa inaongozwa na Afisa Mtendaji Mhandisi Cyprian Luhemeja. 

Akizindua menejimenti hiyo, Profesa Mkumbo amesema kuwa Dawasa mpya inatakiwa kuhakikisha kufika mwaka 2030 wananchi wanapata maji ya kuhakikisha kutokana na ongezeko la watu ambapo Dar es Salaam ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi duniani na ifikapo 2030 ongezeko la watu litafikia takribani Milioni 1. 

Akizungumza katika sherehe za kuunganishwa kwa DAWASA na DASAWCO  Profesa Kitila Mkumbo amesema kuunganishwa huko kutaokoa Sh Bilioni 2.9 kila mwaka zilizokuwa zikipotea katika uendeshaji wa Dawasa na Dawasco na kusema


 fedha hizo zitakwenda kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. 

“Serikali iliamua kuunganisha Dawasa na Dawasco ili kupunguza matumizi na fedha hizi zitaimarisha miundombinu na kuboresha huduma za maji katika eneo la huduma,” alisema Profesa Mkumbo. 

Profesa Mkumbo amewaonya wafanyakazi wa Dawasa mpya kuacha tabia ya ya dharau, nyodo,kukumbatia matatizo, na kuomba rushwa kwa wateja. 


“Baadhi yenu mmekuwa na nyodo, kikola,rushwa na kuridhika na mafanikio kidogo tabia hizi zikome kuanzia sasa,” alisema Profesa Mkumbo. 

Ametaka Dawasa mpya kujiendesha kama kampuni binafsi inayolipwa na wananchi wa Dar es Salaam na si Idara ya serikali ili kuongeza makusanyo ya fedha. 


“Niwaombe mpunguze upotevu wa maji ambao kwa sasa asilimia 47 ya maji yanayozalishwa na Dawasa yanapotea,” alisema Profesa Mkumbo. 

Aidha alisema serikali imeamua kuwapa Dawasa jengo la ghorofa lililopo Ubungo njiapanda ya kwenda Chuo Kikuu ili walimalizie na kuhamia humo. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja ameahidi kuteteleza baakukamilisha miradi mitatu na kutoa muendelezo wa miradi mingine ndani ya siku 100. 

“Zawadi yetu kwa Rais Dk John Magufuli hadi kufikia Disemba 9, mwaka huu tutakamilisha mradi wa maji wa Chalinze, usambazaji wa maji upande wa Goba tegeta na maeneo mengine yaliyokaribu,” alisema Luhemeja. 

amsemandani ya siku 100 hizo watafunga mita za malipo ya kabla nyingi na kuwahakikishia wanaanza ujenzi wa matenki ya Pugu na kusanifu upya mradi wa visima vya Mpera.  


“Ndani y siku hizo pia tutaongeza mapato kutoka Sh Bilioni tisa hadi kufikia Sh Bilioni 12 na pia tutahakikisha tunapunguza upotevu wa maji,” alisema Luhemeja. 









Mwenyekiti wa Bodi wa Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa watashirikiana na menejimenti mya ya Dawasa na watahakikisha kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ya maji kuwafikia wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na Menejimenti mpya ya Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasa) sambamba na wafanyakazi wa Dawasco na Dawasa wakati wa uzinduzi wa Menejimenti hiyo na kumtambulisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto).

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na Menejimenti mpya ya Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasa) sambamba na wafanyakazi wa Dawasco na Dawasa wakati wa uzinduzi wa Menejimenti hiyo na kutambulishwa kwa  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wafanyakazi wa Dawasa na Dawasco baada ya kutambulishwa rasmi kuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo.
 Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo(katikati)  akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili kulia) na menejimenti nzima ya Dawasa.

Wafanyakazi wa Dawasco na Dawasa wakiwa katika uzinduzi wa menejimenti moya ya Dawasa wakifuatilia kwa umakini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad