HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 5 September 2018

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AMEGAWA KOMPYUTA 96 KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA 6

Na Agness Francis,Glogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar Ayoub Mahmoud amekabidhi kompyuta mpakato kwa wanafunzi 96 waliohitimu kidato cha 6 ambao wana ufaulu wa  alama ya daraja la kwanza (devision 1) kwa kila mmoja.

Kompyuta hizo zimetolewa na taasisi ya Mimi na wewe foundation ili kusawasaidia wanafunzi hao kurahisisha kazi katika masomo yao ya elimu ya juu na kuleta hamasa kwa wale waliobaki mashule kufanya vizuri zaidi.

Mahmoud ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa kupyuta hizo  kuwa kiwango cha Elimu kwa mwaka huu kimepanda kulinganisha na kipindi kilichopita.

"hali ya kiwango cha ufaulu katika mkoa wetu haikuwa ya kuridhisha kipindi cha nyuma ambapo tumechukua hatua za dharula na haraka ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kushirikiana na wizara ya elimu,mwaka huu kumekuwa na ongezeko la ufaulu wanafunzi 96 daraja la 1"amesema mkuu wa mkoa huyo.

Katika ugawaji wa zawadi hizo walikuwepo wanamuziki wa aina ya kizazi kipya  waliamsha dude visiwani humo katika viwanja vya mapinduzi square.

Hamsha hamsha hizo zilipamba moto baada ya Mkuu wa Mkoa kumaliza kugawaji wa vifaa  mjini hapo.
 Msanii wa bongo fleva Dogo Janja alivyowapagawisha  wakazi wa visiwani Zanzibar wakati Mara baada ya zoezi la ugawaji wa kompyuta kwa wanafunzi hao katika viwanja vya Mapinduzi Square.
 Wanafunzi wa kidato cha 6 waliofaulu ambao wamehudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika viwanjani mapinduzi square visiwani zanzibar wakati wa  kukabidhiwa zawadi zao.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mahmoud kushoto pamoja na makamu wa  Rais wa Zanzibar balozi seif Iddy Kati kati, wakikabidhi kompyuta mpakato kwa mmoja wa wanafunzi waliofaulu kwa alama ya daraja   la kwanza (devision 1) kidato cha 6 katika viwanja vya mapinduzi square visiwani Zanzibar.
 Msanii wa kizazi kipya  Amba lulu akitoa burudani viwanjani hapo katika kuhitimisha  sherehe za ugawaji wa zawadi za  kompyuta kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha 6  waliofaulu alama ya daraja la kwanza.
Msanii wa muziki wa dansi Papy Kocha akitoa shoo visiwani Zanzibar wakati wa hafla ya ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi hao ambapo mkuu wa Mkoa Wa mjini magharibi Ayoub Mahmoud ndie aliyekabidhi katika viwanja vya Mapinduzi Square.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad