HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 13 September 2018

MATUKIO MBALIMBALI YA SPIKA WA BUNGE LEO JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani Msuya alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani Msuya alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiongoza majadiliano yenye lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi baina ya Makamishna wa Tume ya utumishi wa Bunge dhidi ya Tume ya Baraza la wawakilishi kutoka Zanzibar kikao kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kikao pia kilihudhuriwa na katibu wa Bunge (hayupo kwenye picha) na Watendaji wakuu kutoka pande hizo mbili
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati mwenye tai ya damu ya mzee) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya utumishi wa Bunge na Tume ya Baraza la wawakilishi kutoka Zanzibar baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu  kutoka Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali linaloshirikiana na taasisi za kiserikali katika kupambana vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto  walipomtembela ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali linaloshirikiana na taasisi za kiserikali katika kupambana vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto, Ndg. Sekela Mwakyusa akimtolea ufafanuzi kuhusu shughuli mbali mbali zinazofanywa na Shirika ilo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.  
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye tai mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali linaloshirikiana na taasisi za kiserikali katika kupambana vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto pia linalotoa huduma kwenye mikoa sita ya Geita, Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu. Wajumbe hao walioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Ndg. Asha Mtwangi (wa pili kulia mbele) baada ya kikao kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad