Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 September 2018

Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

Na Frank Mvungi- MAELEZO
Katibu  Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano  kila wanapofanya maamuzi.
Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa  wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
“Nafasi zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.” Alisisitiza Mhandisi Kijazi.
Akifafanua, Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano yakuleta mageuzi makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Aliongeza kuwa Kikao kazi hicho kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila mwaka ili kuwapa fursa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala  kubadilishana uzoefu, kubaini changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa kuzitatua kwa maslahi ya wanachi.
Akizungumzia mabadiliko yaliyofanywa na Serikali Balozi Kijazi amesema kuwa ni pamoja na kuwepo kwa muundo mpya kwa Wizara zote unaoendana na mahitaji na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano utakowezesha kutatutuliwa kwa changamoto zilizokuwepo kabla ikiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Kauli mbiu ya Kikao kazi hicho ni “Uongozi makini na wapamoja unaozingatia uzalendo, uwajibikaji, utawalabora na kusimamia rasilimali zetu ni nyenzo muhimu katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa Kati” Alisisitiza Balozi Mhandisi  Kijazi.
Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara, Makatibu Tawala wa Mikoa Kinafanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kikilenga kuimarisha na kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akifungua  Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Mtendaji Mkuuwa Taasisi ya Uongozi Prof.   Joseph  Semboja akisistiza jambo wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Sehemu ya Makatibu Wakuu wakifuatilia uwasilisjhaji wa mada mbalimbali  kwenye Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini  Bw.  James Syanga akiwasilisha mada kuhusu athari za madawa ya kulevya wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
  Manaibu Katibu Wakuu  na  Makatibu Tawala wakifuatilia mada wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma. (Picha zote na Frank  Shija- MAELEZO)
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi akijitambulisha wakati wa wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw. David Kafulila akijitambulisha  wakati wa wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.  Nichalaus William akijitambulisha katika kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John  Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu  mara baada ya kufungua  kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.
  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John  Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa mada wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018 wakiwemo Makatibu Wakuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad