HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 25, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AWAASA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA NIDHAMU YA HALI YA JUU

LUSUNGU HELELA-DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ametoa rai hiyo leo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu

Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi ameelezea kufurahishwa kwake na ushirikiano alioupata kutoka kwa watumishi wa Wizara hiyo na kuelezea kuwa, ndio umemwezesha kuiongoza vema wizara hiyo kwa kipindi alichokuwepo madarakani na kupelekea mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Wanyamapori, Utalii, Misitu na Nyuki na Malikale.

Ameongeza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya ujangili ambayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri uliopatikana kutoka kwa watumishi wa Wizara, wananchi, Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa Wanyamapori.

“Katika Kipindi tulichokuwa pamoja, kuna mambo mengi tumeyakamilisha. Nimefanya kazi nanyi na kila mmoja wenu alikuwa akinisaidia ili Wizara yetu iweze kusonga mbele. Hakuna hata mmoja aliyeonyesha kutaka kunikwamisha. Ninawashukuru sana”Amesema Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa UDOM jijini Dodoma na kuhudhuriwa na watumishi wapatao 113 wa Wizara hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aloyce Nzuki, amempongeza Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi kwa kustaafu rasmi jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Amemsifu Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi kwa umahiri wake katika utendaji hasa namna alivyoweza kufanya kazi na raia kwa ushirikiano wa hali ya juu wakati yeye ni Mwanajeshi.

“ Umefanya mambo makubwa kwa kuweka mifumo mizuri pamoja na kubuni mikakati na mbinu za kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Wizara kiutendaji na kuhakikisha watumishi wanapata utulivu wa akili kwa kujali maslahi ya watumishi na haki zao na hivyo kuwawezesha kufanya kazi wakiwa na utulivu wa akili jambo liliongeza ufanisi katika kazi.”ameelezea Dkt. Nzuki.

Akitoa Shukrani kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa Dkt. Nzuki wakati akiiongoza Wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi amesema, amepata ushirikiano
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kulia) akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati akiwaaga leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu ambapo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki.
 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili wakiwa wamesimama kwa muda wa dakika moja mara ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara kabla ya kuzungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kwa ajili ya kuwaaga leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu. .
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kushoto) akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) mara baada kumaliza kuwaaga Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( wa pili kushoto) akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki (wa kwanza kushoto) akiwasili kwa ajili ya kuwaaga Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu ambapo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Wengine ni Wasaidizi wake.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad