HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 7, 2018

KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya soka ya ufukweni (Beach Soccer) Boniface Pawasa amesema kuwa kwa sasa anavunja kambi rasmi siku ya Jumapili kwa ajili ya wachezaji kurudi nyumbani baada ya wapinzani wao Afrika Kusini kujiondoa kwenye mechi ya kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON  Nchini Misri.

Akizungumza leo, Pasawa amesema kuwa kambi waliyokuwa wameweka na wakiendelea na mazoezi kwenye Fukwe za Coco Beach ilikua ni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ho na Afrika Kusini ambapo wamejitoa tayari.

"Lengo letu la kwanza ilikuwa ni mechi dhidi ya Afrika Kusini lakini wamejitoa tayari ambao ulikua  ni mchezo wa kufuzu kwenda Mataifa Afrika (AFCON) na tutawalipa wachezaji wote stahiki zao ili warejee majumbanu," amesema Pawasa.

Amesema, katika maandalizi yajayo kwa ajili ya michuano ya  kuwa wameshatuma maombi kwa  timu ya Taifa ya Oman  kwa Kocha Talib Hilal  kwa ajili ya kuweza kupata kambi ya wiki mbili kabla ya kwenda nchini Misri kuchuana katika michuano hiyo ya AFCON.

"Wenzetu Oman ni wazoefu wameweza kucheza hata mashindano ya dunia kwahiyo kupata nafas ya wiki mbili nchini mwao itakuwa ni nafasi nzuri sana kwetu kwa maandalizi ya AFCON, ukiangalia Oman na Misri sio mbali,"amesema.

Pawasa amesema kuwa mpaka sasa ameshaomba mechi za kirafiki kwa timu ya Malawi na Uganda kwa ajili ya kupata mchezo wa kirafiki kujiandaa na michuano ya AFCON miezi mitatu ijayo.

kIkosi cha timu ya Taifa ya soka la Ufukweni wakiwa katika picha ya pamoja.

micAmeeleza kuwa  mbali na hilo atakuwa na programu ya kuweza kuwapata wachezaji wengi wa mchezo huo mwezi Oktoba mwaka huu na kuwataka wachezaji wa mpira wa miguu kuja kutafuta fursa baada ya kushindwa kuoata nafasi kwenye timu ya taifa ya mpira wa miguu.

Mbali na hilo, Pawasa amewaomba watanzania waweze kujitokeza kuisaidia timu ya taifa ya soka la ufukweni kwani ni timu inayowakilisha nchi na sio klabu, wasiwaachie majukumu yote Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwani imechukua miaka takribani 30 kuweza kufuzu kwenda Michuano ya AFCON na malengo yakiwa ni kuhakisha wanapata nafasi ya kwenda Kombe la Dunia nchini Paraguay.



Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali za Africa zitakazofanyika nchini Misri. 
 baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha barua ya kujiondoa katika mashindano.  


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tayari wametuma barua hiyo ya kufuzu kucheza Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi Nane.

Timu ya  Soka la Ufukweni ilikuwa kambini kujiandaa na mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili Septemba 9,2018 na kambi hiyo itavunjwa rasmi Jumapili.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Soka la Ufukweni wakiwa katika mazoezi Fukwe za Coco Beach.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad