HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 6, 2018

DC CHAMWINO AMKARIBISHA OFISA TARAFA ALIYEKUWA MASOMONI CHINA, AMUAHIDI USHIRIKIANO

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Vumilia Nyamoga amempongeza Ofisa Tarafa wa Itiso Remidius Emmanuel.

Pia amemkaribisha tena  kuendelea na majukumu yake ya kutumikia Taifa ikiwa ni siku chache  tu baada ya kurejea nchini akitokea masomoni nchini China.

"Wilaya ya Chamwino inakutegemea sana na tunatarajia maarifa uliyoyapata yataleta tija zaidi,..Ninakuahidi ushirikiano popote pale utakapohitaji msaada zaidi nitakuunga mkono,"amesema Vumilia

Pia amemtaja Remidius kama Ofisa Tarafa machachali na mchapa kazi na kuwataka Viongozi, watendaji  wa tarafa ya Itiso kumpatia ushirikiano wakati ambo amerejea kwa ajili ya kuwatumikia.

Kwa upande wake Remidius, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa namna ya kipekee kwa shauku ya mapokezi makubwa.

Amesema baada ya  kurejea kutoka masomoni amekuja kukutana na Kufanya mazungumzo na Mkuu wake wa kaziMkuu wa Wilaya.

Amesema amemueleza machache aliyojifunza na kwamba tayari ameanza kazi.

" Ninaahidi kuendelea kutumia uzoefu na maarifa ya kile nilichojifunza nchini China kwa ustawi na maendeleo ya Taifa langu  kupitia Tarafa ya Itiso,"amesema.

Katika hatua nyingine Remidius alimkabidhi Mkuu huyo Kitabu kinachoeleza historia na mifano kutoka baadhi majimbo nchini China  yalivyoweza  kujikwamua na janga la umasikini (The way Forward: Stories of Poverty Reduction in China) 
Amesema kuwa "Kitabu hiki kinaeleza namna ambavyo Taifa la China limeendelea kufanikiwa katika mapambano dhidi ya umaskini, mapambano hayo ndio ambayo hata sisi (Tanzania) tunaendelea nayo.

" Na sasa tunao mwelekeo wa kuufikia Uchumi wa wakati 2025 zote ni juhudi za kuondoa umasikini....naamini hii ni zawadi sahihi kwa mkuu wangu na yeye amefurahia sana, kupitia uzoefu uliomo naamini Chamwino itasonga mbele zaidi,"amesema Remidius

Juni 29 mwaka 2018  Chuo Kikuu cha Kilimo nchini China (China Agricultural University - CAU) kilimtunuku Cheti Maalum akiwa ni mwanafunzi pekee kutoka Afrika  katika chuo hicho kama "Outstanding Graduate "

Ikiwa ni kutambua juhudi zake katika kujituma na mtu mwenye bidii kwa kipindi chote akiwa masomoni.

Remidius  Emmanuel ambaye pia alikuwa ni katibu Mkuu wa Shirikisho la wanafunzi Watanzania nchini China aliweza kutembelea zaidi ya majimbo 15 katika taifa hilo na kujifunza mambo mbalimbali kutoka taifa hilo.

Mapema Julai mwaka 2018  alichaguliwa kushiriki katika kambi maalum ya Vijana nchini China ("Future Leader and  Youth Ambassador, International Social Practice Summer Camp") Julai 16 mpaka Julai 22 Julai,2018.

Ambapo ilihusisha vijana  wapatao 140 (International & Chinese Students) kwa uwakilishi wa vyuo vikuu jijini Beijing, China akiwa mtanzania pekee aliyeshiriki katika kambi hiyo iliyofanyika katika Jimbo la Hebei ( Eneo jipya la Xiongan)

Itakumbukwa  Aprili 1 mwaka  2017, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jiping (Kupitia Kamati kuu ya Chama cha Kikomunist cha China - CPC ) aliutangaza mji wa Xiongan (katika Jimbo la Hebei) kama eneo jipya " Xiongan New Area".

Mji ambao ifikapo mwaka 2035 utakuwa ndio mji wa kisasa zaidi ya miji ya Shenzhen (Jimbo Guandong) na Pudong (Jimbo la Shanghai) na China kwa ujumla kama Ukanda maalum mpya wa kiuchumi (New Special Economic  Zone).

Wengi wamemtaja kijana huyu kama sehemu ya vijana wachache ambao wanajituma kwelikweli na wenye hulka za uzalendo kwa Taifa.
Ofisa Tarafa wa Itiso, Remidius Emmanuel(kushoto) akifafanua jambo mbele ya Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga kuhusu Kitabu hicho kinachoelezea mapambano ya Umasikini kwa mifano ya baadhi ya maeneo nchini China alipokuwa masomoni nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad