HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 5, 2018

CHAMA CHA WAAJIRI WAANZA MAFUNZO KUNDI LA TATU LA PROGRAMU YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wameanza kutoa mafunzo ya kundi la tatu kwa wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) wakishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation Of Norway Enterpise NHO) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yatakayokuwa katika kozi tatu yanalenga zaidi katika kuwapa mwongozo bora wafanyakazi wa kike ili waweze kumudu nafasi zao za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa wameshasajili wafanyakazi wa kike 24 kutoka makampuni 11 ambayo yamefadhili mafunzo hayo na kundi hili ni la tatu toka waazne kutoa mafunzo hayo na tayari wanawake 60 wameweza kupata programu hiyo.

Dkt Mlimuka amesema mafunzo haya yatachochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya kampuni na yatawapa ujasiri wanawake kuomba nafasi za uongozi sehemu mbalmbali ikiwemo bodi ya wakurugenzi..

Amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano na katika maisha yao kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (
ESAMI) kwa muda wa siku 14 muda wa darasani kwa kozi zote tatu ndani ya miezi tisa na yatafanyika kwa mfumo wa kuunganishwa na shughuli za kila za muhusika mahali pake pa kazi.

" Tumewasajili wahitimu wote kama wafanisi wa bodi za wakurugenzi na uongozi, ujuzi hui utaendelezwa katika kizazi cha baadae lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na mazingira bora ya kazi," amesema.

Dkt Mlimuka aliongeza kuwa ATE inatambua ushiriki kutoka makampuni hayo kama chachu ya kuendeleza mipango mikakati katika usawa, elimu bora na mazingira bora ya kazi katika kuinua uchumi wa nchi.

Mbali na hilo amesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano wa pamoja kwa wanawake wote waliofanikiwa kupata mafunzo hayo kuona wamefikia wapi kabla na baada ya kupata programu ya mwanamke wa wakati ujao pia hafla hiyo itatoa mwongozo wa mwendelezo wa kila mwaka kuwa na makongano hayo. 

Programu huu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) ilizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu mwaka 2016 ambapo ililenga zaidi kuongeza ufanisi kwa waajiri wa kike mahali pa kazi pamoja na mambo mengine ilibanishiwa kuwa wahusika wataunda mtandao wa kubadilishana uzoefu katika fani mbalimbali.

Makampuni yaliyoshirikiana na ATE ni Barclays Bank Tanzania, Commercial Bank of Africa, Equinor Tanzania AS, Global Health Program- Tanzania (HJFMRI), Grumeti Reserves, Kilimanjaro Airports Developments Co. (KADCO), Legal and Human Rights Centre (LHRC), National Housing Corporation (NHC), Social Action Trust Fund (SATF), Standard Chattered Bank na TOL Gases Ltd.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya mwanamke wa wakati ujao (Female in future) yenye malengo ya kumpa fursa mwanamke 
juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano 
wakati akizindua leo Jijini Dar es Salaam. Chini akizungumza na wanahabari.




Mhadhiri mwandamizi wa




Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Apollonia Kerenge akizungumza na wanawake waliokatika mafunzo ya mwanamke wa wakati ujao (female in future) iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya wanawake wa wakati ujao (female in future) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad