HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 13, 2018

ABIRIA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI WASHAURIWA KUTOA TAARIFA ZAO KWENYE MAMLAKA SAHIHI BADALA YA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Richard Mayongella  amewataka abiria wanaotumia viwanja vya ndege kusafiri maeneo mbalimbali kuacha kukimbilia kwenye mitandao pindi wanapobaini kuna upotevu wa vitu.

Amewataka kutumia mamlaka husika  katika uwanja huo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kamili ya jambo linalolalamikiwa.

Mayongella ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusambaa kwa taarifa ya abiria aliyotumia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kudai ameibiwa wakati ukaguzi wa mwisho

Amesema katika viwanja vya ndege kuna vitengo mbalimbali ikiwemo kituo cha polisi, hivyo kama kuna abiria anaibiwa mizigo au chochote basi ni vema kuripoti kwanza kwenye vyombo hivyo ili kuruhusu kufunguliwa jarada la uchunguzi na si kwenye mitandao ya kijamii na kuchafua taswira ya nchi.

Mayongella amesema kuwa abiria huyo alikuwa anasafiri kuelekea ughaibuni  nakudai kuibiwa pochi yake katika Uwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Julius  Nyerere.

 Alikiri kuwa Septemba 8 mwaka huu abiria huyo jina wanalihifadhi alikuwa anasafiri na ndege aina Emirates lakini wakati anafanya taratibu za kufanyiwa ukaguzi na kumalizika baadae akaja nakudai ameibiwa pochi.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwa mujibu wa abiria huyo ambaye pia ni mtanzania anayeishi Ughaibuni baada ya kutokea kwa tukio hilo aliaza kulalamika na kuuliza wakaguzi uwanjani hapo huku akilazimisha kuangalia kwenye Tv kamera ili kubaini aliyeibwa pasipo kufuata utaratibu.

"Ndugu zangu waandishi wa habari nataka kusema ni vema abiria anapoibiwa au kupotelewa na kitu chake hatua ya kwaza lazima uripoti katika kituo chetu cha Polisi ambacho kipo hapa kiwanja ili kutoa maelezo na kufunguliwa jarada kwa ajili ya upelelezi.Si  kukimbilia kuchafua kupitia mitandao ya kijamii,"amesema

Hata hivyo akimzungumzia abiria huyo ambaye ni mtanzania amesema jambo ambalo amelifanya si jambo jema ukizingatia yeye ni mtanzania alipaswa kuonesha uzalendo huku jambo lake likifanyiwa upelelezi badala ya kusambaza ujumbe kwenye mitandao ambao kimsingi unasomwa duniani kote.

Amesema  baada ya kuona ujumbe huo  kwenye mtandao wao kama mamlaka ilibidi watafutwe ndugu wa abiria huyo ambao ni watanzania ili kuzungumzia jambo hilo nakuwataka ndugu hao kuwasiliana na ndugu yao ambaye alishasafiri ili atoe ushirikiano  kwa mamlaka.

"Tupo hapa na ndugu wa abiria wetu ambaye unadaiwa wakati anasafiri siku hiyo ya Alhamisi ,Septemba 8 mwaka huu  ili kuzungumzia jambo hili na msingi tumelazimika kuonesha hadi Tv Kamera mbele yao na hapa kwenu waandishi tutawaonesha ili muone kama kweli madai ya kuibiwa kwake hapa kuna ukweli japo Tv Kamera zetu hazionyeshi wizi huo,"amesema Mayongella

Amesema abiria huyo aiombe radhi Mamlaka na bila kufanya hivyo hata zitachukuliwa dhidi take.

Kwa upande wa ndugu ambaye alijitambulisha kuwani Wael Akrab yeye amesema wao kama ndugu hawawezi kuzungumzia zaidi tukio hilo kwasababu muhusika mkuu hayupo na ndo aliyetuma ujumbe huo .

Akrabi amesema pia wanashukuru kwakuwa wameona hadi kwenye kamera katika kila hatua ambayo ndugu yao alipita ila japo wameona hawawezi kueleza chochote na kwamba wataendelea kuwasiliana na ndugu yao ili kuweza kuomba radhi hiyo.

Kwa upande wa waandishi wa habari nao walipata fursa ya kuonyeshwa kamera zinavyofanya kazi uwanjani hapo lakini pia abiria anayedaiwa kuibiwa jinsi alivyokuwa anakaguliwa  huku wakitoa ushauri wa maboresho ya kiukaguzi katika kiwanja hicho kikubwa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela (katikati)  akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shutuma za wizi wa pochi kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBII).
Bw. Wael Hassan (kulia) akiushukuru uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwa kuonesha picha zilizopigwa na kamera za Usalama za tukio la kulalamikiwa kwa wizi wa pochi ya dada yake (jina limehifadhiwa), aliyesafiri tarehe 8 Septemba, 2018 akielekea Dubai.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad