HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 3, 2018

WANAWAKE KUNUFAIKA NA HUDUMA YA HEDHI SALAMA KIMTANDAO

     Na Khadija Seif,Globu ya jamii

Washiriki wanaowania taji la Ulimbwende kwa mkoa wa Dar es salaam, wametakiwa kuzungumza na wanawake hasa wasichana wadogo na kusambaza elimu kuhusu hedhi salama ili kupunguza na kutokomeza mimba za utotoni na zisizotarajiwa pamoja na matatzo ya afya ya uzazi kwa ujumla
Hayo yamebainishwa leo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries Flora Njelekela,alipokuwa akizungumza na warembo mbalimbali kuhusu Afya ya uzazi pamoja na hedhi salama.
Njelekela Alisema kuwa kwani wasichana wengi wamekua wakipitia changamoto ya kupata maumivu makali pindi wanapoingia kwenye hedhi zao.

"Nimekutana na walimbwende na kuwapa machache kuhusu huduma ya hedhi salama itakayowafikia wahitaji kwa njia ya mtandao, ambayo itawasaidia wanawake kujua mzunguko wao wa hedhi na afya kuhusu hedhi salama,kuepuka mimba zisizotarajiwa na pia itawapa fursa kuongea na mdaktari kuhusu afya ya uzazi",alisema Njelekela.
Alisema kuwa huduma hiyo itawasaidia wanawake kufanya vipimo vya hedhi pamoja vipimo vingine vya saratani ya matiti .
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries, Flora Njelekela akifafanua kuhusu namna ya kujifunza mambo mbalimbali ya afya kwa njia ya mtandao.Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries,Flora Njelekela akifafanua jambo mbele ua Warembo mbalimbali leo jijini Dar as Salaam kuhusu afaya ya uzazi pamoja na hedhi salama,pichani kulia ni Mkurugenzi Msaidizi,Carolyne Njung’e.Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries, Flora Njelekela akiwa katika picha na warembo leo jijini Dar as Salaam.picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad