HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 29, 2018

WACHEZAJI SITA WA SIMBA WAONDOLEWA TIMU YA TAIFA

Kikosi cha Taifa Stars.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Emmanuel Amunike amewaondoa kikosini wachezaji Sita(6) wa klabu ya Simba na mchezaji mmoja(1) wa klabu ya Yanga kwa kushindwa kuripoti kambini. 

Wachezaji walioitwa kwenye timu ya Taifa walitakiwa kuripoti Jumatatu jioni Agosti 27,2018 isipokuwa wachezaji wa Yanga wanaokabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na wale wanaocheza soka nje ya Tanzania.

Wachezaji walioondolewa kikosini ni Erasto Nyoni,Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Ramadhan Kichuya,John Bocco,Hassan Dilunga wote Simba na Feisal Salum wa Yanga.

Feisal ameondolewa kwa kushindwa kuripoti kambini kwa kuwa hakuongozana na klabu yake ya Yanga kwenda nchini Rwanda kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza mashindano hayo hivyo alitakiwa kuripoti kambini kama alivyotakiwa. 

Wachezaji walioitwa kuziba nafasi hizo ni 
Salum Kimenya(Tz Prisons)Paul Ngalema,(Lipuli),Frank Domayo(Azam FC),Salum Kihimbwa(Mtibwa),Kelvin Sabato(Mtibwa)David Mwantika(Azam FC) na Ally Abdulkarim(Lipuli)

Wachezaji hao wanaungana na wengine walioitwa Taifa Stars kukamilisha kikosi cha wachezaji 25.

Wachezaji wengine walioitwa awali ni 
Aishi Manula(Simba)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Yanga)
Hassan Kessy (Nkana)
Gadiel Michael (Yanga)
Abdi Banda (Baroka)
Kelvin Yondan (Yanga)
Aggrey Morris Lipuli(Azam FC)
Andrew Vicent (Yanga )
Himid Mao (Petrojet)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida)
Rashid Mandawa (BDF)
Farid Mussa (Tenerife)
Feisal Salum (Yanga)
Mbwana Samatta (Genk)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal)
Shabani Chilunda (Tenerife)
Yahya zaydi(Azam FC)

Wachezaji walioingia kambini hotel ya Sea Scape wanaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans chini ya kocha Mkuu Emmanuel Amunike na wasaidizi wake Hemed Morocco na Emeka Amadi. 

Tayari kati ya wachezaji 7 walioitwa kuchukuwa nafasi za walioondolewa wamesharipoti kambini na kuanza mazoezi na wenzao.

Wachezaji walioripoti baada ya kuitwa leo ni Frank Domayo na David Mwantika wote wa Azam FC.

Wakati huohuo viongozi wa klabu ya Simba Kaimu Katibu Hamisi Kisiwa na Meneja wa timu hiyo Richard Robert watafikishwa kwenye kamati ya maadili ya TFF kwa kukiuka maagizo halali ya TFF na kushindwa kuhakikisha wachezaji wao wanaripoti kambini huku wakifahamu taarifa hiyo iliyowafikia kimaandishi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad