HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 6, 2018

Vodacom yadhamini na kutoa vifaa vya mawasiliano kwa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro

 Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (katikati) akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Samsung kanda ya Africa Sung Yoon (kushoto) aliyeambatana na mwanaye Jason Yoon  baada ya kuwakabidhi Moderm zitakazotumika kwa ajili ya mawasiliano wawapo mlimani, zoezi hili hufanyika kila mwaka  kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watoto wa kike ijulikanayo kama Trek4Mandela.
 Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi na rais mstaafu wa taifa la Afrika Kusini ijulikanayo kama Trek4Mandela wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro. Zoezi hili hufanyika kila mwaka kwa udhamini wa kampuni ya Vodacom na pesa zinazokusanywa hupelekwa kusaidia vifaa vya Wasichana kujistiri pindi wanapokuwa kwenye hedhi.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen akikabidhi Moderm kwa mmoja wa washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Trek4Mandela,wakati washiriki hao wakiagwa kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda Mlima, Vodacom imekabidhi Moderm sita kwa kundi hilo ili kurahisisha mawasiliano wakati wa kupanda mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad