HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 4 August 2018

RIDHIWANI AISHUKURU SERIKALI KWA JITIHADA ZA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KARIBU KWA WANANCHI JIMBONI CHALINZE

 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ameishukuru Serikali kwa kuipatia Halmashauri ya Chalinze Sh.bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo ya Kibindu,Mkange na Lugoba kwa lengo la kusogeza huduma za afya kwa wananchi.

Ridhiwani ametoa shukrani wakati akipokea msaada wa vifaa vya ofisi kutoka Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support ambapo amesema fedha hizo zimetolewa katika kutekeleza mpango wa kujenga vituo vya afya katika halmashauri ya Chalinze.

Amefafanua na kwa sasa kituo cha afya Kibindu kimepatiwa Sh.milioni 420 na kituo cha afya Mkange kimepata katika hatua za mwisho kukamilika na Sh.milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Lugoba.
Amesema kuwa mpaka sasa Serikali imetoa madaktari 47 kwa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na lengo ni kupunguza tatizo la uhaba wa watoa huduma ya afya na Katika Hospitali ya wilaya Msoga  ambapo watapata madaktari 10 ili kuimarisha huduma.

Ridhiwani amesema msaada huo wa Serikali ni mkubwa kwa wananchi wa halmashauri ya Chalinze katika suala zima la kupata huduma za afya na kielelezo kinachoonesha jinsi gani Serikali imekuwa bega kwa began na wananchi katika kuhakikisha wananchi hawatembei umbali mrefu kupata huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wa Mwakilishi wa THPS, Sisty Moshi amesema taasisi yao kupitia usaidizi wa Serikali ya Marekani imekuwa inasaidiana na Serikali katika utoaji wa huduma ya afya.

Ambapo kwa sasa imekuwa ikijihusisha katika utoaji wa huduma katika mikoa ya Kigoma, Pwani na Zanzibar na ikijielekeza zaidi katika utoaji wa huduma ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi katika utoaji wa huduma na tiba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad