Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege ya Rais tayari kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulikwenye kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu
Philip Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Mhe.
John Momose Cheyo wakiwa ndani ya ndege ya Rais kabla ya kuondoka
kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais
mteule wa nchi hiyo Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo
Jumapili Agosti 26, 2018. Katika safari hiyo viongozi hao wanafuatana
na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo
pichani) ambaye atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment