HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 29, 2018

NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA DAR KUTATUA CHANGAMOTO ZA USARISHAJI MIZIGO

 Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya semina iliyohusu kubadilishana uzoefu wa usafirishaji wa mizigo barani Afrika.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Usaje Asubisye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya semina ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu usafirishaji wa mizigo kati ya nchi moja na nyingine barani Afrika.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
NCHI wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wamekutana Dar es Salaam kujadili na kubadilishana uzoefu wa kutatua changamoto hasa wanazokutana nazo katika usafirishaji mizigo kati ya nchi moja na nyingine.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Usaje Asubisye wakati anafungua semina kwa washiriki wa nchi hizo.

Amefafanua msingi wa kukutana kwao ni kujadili kwa kina kutatua changamoto zilizopo na lengo lao ni kuhakikisha nchi za Afrika zinashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi.

Ametaja baadhi ya nchi ambazo zimeshiriki semina hiyo ni Rwanda,Afrika Kusini ,Kameruni,Every Coast na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amesema kuwa pamoja na mambo mengine watajadili namna ya kuboresha utoaji huduma ya kusafirisha mizigo na kwa Tanzania nayo itatoa uzoefu wake na namna ambavyo wamefanikiwa kuondoa changamoto.

“Afrika tunataka liwe bara ambalo litakuwa na uchumi imara na hivyo kwetu sisi kupitia semina hiii tutaangalia nini kifanyike ili tupige hatua,”ameongeza.

Ameeleza pia nchi za Afrika ambazo zinabandari kuweka mkakati sahihi wa kusaidia nchi nyingine katika kusafirisha mizigo.

Pia amesema kuna baadhi ya changamoto ambazo zipo katika nchi moja na nyingine hakuna kutokana na uwepo wa masuala ya sharia, hivyo kupitia semina hiyo wataangalia namna ya kutua baadhi ya kero ili kurahisisha usafirishaji bidhaa katika nchi hizo.

Kuhusu mafanikio Asubisye amesema awali  kwa Tanzania usafirishaji wa mizigo kutokea bandari ya Dar es Salaam hadi nchini Rwanda zilikuwa zinatumika siku 12 lakini kwa sasa ni siku tano.

Akizungumzia zaidi changamoto ambazo wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi wake ni kwamba TRA inataka kuona idara na mamlaka za Serikali zinafanya kazi kwa pamoja.

Amefafanua kwa sasa unaweza kukuta TRA wametoa kibali mzigo usafiri lakini anapofika barabarani mzigo unazuliwa kwasababu ya kuzidi au askari wa usalama barabarani nao wanakuwa na mambo yao na hivyo kusababisha usumbufu.

Hivyo katika kushughulikia hilo wanataka wote ambao wanahusika wanafanya kazi kwa pamoja kwani kuzuia mzigo kunasababisha kuongezeka kwa gharama na athari zake zinamkuta mtumiaji wan chi nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad