HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 26 August 2018

MBUNGE CCM ACHARUKA UBADHIRIFU ULIOFANYIKA JIMBONI KWAKE

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa jimbo la Manonga, Mh. Seif Gulamali ambaye siku za karibuni amegeuka mwiba mkali kwa watendaji wabadhirifu ndani ya wilaya ya Igunga na hii ni baada ya kuona kasi ya watendaji wake ikiwa legevu, na  wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mh.Kasimu Majaliwa Jimboni humo Mbunge huyo aliibua ufisadi wa zaidi milioni 170, na Waziri Mkuu aliagiza wahusika wote kukamatwa.

Leo akizungumza na blogu ya jamii Gulamali ameeleza mwenendo na msimamo wake katika kuhusu azma yake ya kuleta mandeleo Jimboni humo.

Gulamali ametoa angalizo kwa watendaji wa kijiji cha Kijiji cha Bulangamilwa na kusema kwamba; "Zimepotea Milioni 141 na Mifuko 90 ya saruji katika Kijiji hicho licha ya  kupata shilingi Milioni 700 za Mradi wa Maji ambao umetekelezwa chini ya kiwango na Maji hayatoki, huo ni Ubadhirifu tena wa Fedha za Umma. Siwezi kunyamaza" amesisitiza.

 Akieleza kuhusu sakata la Kijiji cha Choma Mbunge Gulamali amesema; "Zimetolewa Milioni 35 za Mashine ya Mpunga na badala yake ikanunuliwa  mashine iliyotumika na mpaka leo hakuna kinachoendelea. Nilipiga sana kelele juu ya masuala haya lakini waliweka nta kwenye masikio huku wakiendelea kunibeza wakitumia nafasi zao kuwalinda wezi, nimeomba kuwatumikia Wana Manonga na wakaniamini kwa Miaka 5 nitahakikisha fedha zenu za Miradi ndani ya Miaka yangu 5 hazipotei kirahisi tutakula nao Sahani Moja. Narudia tena, haitapotea hata mia moja nikanyamaza"amesisitiza Gulamali.

Kuhusu watendaji wanaofanya kazi chini ya viwango Gulamali amesema kuwa; "kwa wale ambao wanawaza kufanya kazi chini ya Viwango ndani ya Jimbo langu hao hawana nafasi na wasipoteze muda wao kwani watarudia kazi zao mpaka wakae sawa"ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa anashukuru Mungu kwa kuwa  hadi sasa ahadi alizotoa nyingi zimekamilika na chache zipo katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Gulamali ameeleza kuwa Ubunge sio Ufalme, Udikteta wala Usultani ni Utumishi  na aliomba kuwatumikia wana Manonga kwa Miaka 5 na aliwaambia wapiga kura wake kuwa  akishindwa kutimiza Ahadi alizotoa wampige chini.

"Niliahidi na Ninatekeleza, Sina Muda wa Kuupoteza" Gulamali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad