HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 2, 2018

Maamuzi ya taasisi lazima yashirikishe baraza la wafanyakazi –Profesa Msanjila

Na Chalila Kibuda
Maamuzi yanapotakiwa kufanyika ni lazima uwepo ushirikishaji ili kuweza  kuendesha taasisi na kupata mafanikio ya kimaendeleo na taifa kuona tija ya tasisi husika.

Hayo aliyasema  Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila wakati akifungua Baraza la Pili la Shirika la Taifa la Madini (Stamico) amesema sheria ya mashauriano katika utumishi wa umma, serikali imebainisha nia yake thabiti ya kutaka kuona wafanyakazi wakishirikishwa  katika kusimamia na kuendesha taasisi wanazozimamia.

Amesema kuwa baraza ni chombo muhimu katika taasisi hivyo lazima kitumike katika  kujadili mambo mbalimbali yanayoyohusu masilahi na ustawi wa watumishi , mipango  na malengo ya kazi ya kuishauri menejimenti ya Stamico.

Profesa Msanjila amesema  viongozi waliochaguliwa katika baraza  la wafanyakazi wa stamico kunadhihirisha imani ya wafanyakazi kuwa kile wanachokitaka kitafanyika kutokana na maamuzi ya ushirikishwaji.

Nae  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Stamico Mhandisi Kanali Sylvester Ghuliku amesema baraza lilopita lilikuwa na changamoto nyingi ambazo zilikuwa zinatokana na shirika lenyewe kwa kutokuwa na fedha za kuitisha mkutano wa baraza na fedha ambazo zilikuwa zinapatikana katika shirika kidogo na hata kuendesha ofisi hazikutosha.

Amesema kuwa baraza litafanyaka kazi katika misingi iliyowekwa katika uanzishaji katika kufikia lengo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akizungumza na baraza jipya la wafanyakazi  la pili la Stamico lilofanyika Ofisi za Stamico jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akiwa na wafanyakazi wakiimba wimbo wa mshikamano
 Watoa maada kutoka ofisi ya Kamishina wa madini, , Idara ya kazi na wawakilishi kutoa Chama cha wafanyakazi wa Migodi, Nishati , Ujenzi na Kazi Nyinginezo (Tamico)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila wa sita kutoka  kushoto mstari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la pili jipya la Wafanyakazi wa Stamico, kulia kwa katibu Mkuu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Stamico Mhandisi Kanali Sylvester Ghuliku wane kutoka kushoto mstari wa mbele ni Katibu Mpya wa Baraza hilo Juma Mbawambo
 .Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akisalimiana katibu mpya wa baraza la wafanyakazi la pili la Stamico Juma Mbawambo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad