HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 August 2018

KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA HAMAI

KATIBU tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi ametembelea katika kijiji cha Hamai kukagua ujenzi wa zahanati ya Hamai inayojengwa na wananchi wa kijiji hicho na kusikiliza changamoto zao, pia ametoa vifaa vya ujenzi na kushiriki kufanya baadhi ya kazi za ujenzi wa zahanati hiyo.

Akizungumza na Mafundi ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai amesema kuwa zahanati hiyo inatakiwa imalizike kwa haraka na kwa ufanisi mzuri ili kusaidia wananchi kupunguza kilometa za kutembea kwaajili ya kutafuta huduma mhimu ya kijamii ya afya.

Pia wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji amewaongezea wahandisi wa ujenzi na kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi ambavyo ni Mbao, misumari chokaa pamoja na tiles. 


 Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
 Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akitembelea  ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi  ametoa vifaa vya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma vifaa hivyo ni pamoja na mbao, tiles chokaa na misumari.
 Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akisaidia kupaka rangi kwenye jengo la zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akizungumza na wajenzi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma mara baada ya kutoa mchango wa vifaa ya ujenzi pamoja na kuwaongezea wahandisi wa ujenzi kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo la zahanati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad