HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 August 2018

Dkt.KIJAJI AFUNGUA MKUTANO 41 WA BIMA KUTOKA NCHI 39 MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA(OESAI)


Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji akizungumza katika mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) Picha na Vero Ignatus.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha.
Wapili kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, aliyepo kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware, akifuatiwa na Rukia Adam Mjumbe kutoka (TIRA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka baadhi ya matataifa 39 Duniani. Picha na Vero Ignatus.

Na.Vero Ignatus.Arusha
Mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) umefunguliwa leo rasmi mkoani Arusha.

Mkutano huo umefunguliwa na Naibu waziri wa fedha Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameyataka makampuni ya Bima kutoa huduma za Bima kwa wakulima ili kufikia uchumi wa kati.

Dk, Kijaji amesema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu kuhusu bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati.

Ameyataka makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima.

Amesema watanzania wanaotumia bima hapa nchini ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za Taifa.

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware amesema mkutano huo wa 41 unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje za bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi.

Aidha amesema kampuni hizo zitapata fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa Tehama unaoleta mageuzi katika utoaji wa huduma bora zako bima, rasilimali watu na kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali kwaajili ya kulipia bima ya maisha.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman amesema lengo la mkutano huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 50 ya watanzania wawe na aina yoyote ya bima kwani kwa sasa Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za bima

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad