Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga wameendelea kusalia kwenye nafasi ya mwisho ya Kundi D baada ya kukubali kichapo cha golo 3-2 kutoka kwa Gor Mahia ya Nchini Kenya.
Mchezo huo uliochezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ilichukua dakika moja kwa Gor Mahia K'Ogalo kuandika goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake George Odhiambo Ogutu baada ya kumalizia mpira uliotemwa na golikipa Youthe Rostand.
Yanga wakiwa wanajaribu kutuliza kasi ya Gor Mahia pamoja na kusaka goli la kusawazisha lakini katika dakika ya 41 kupitia kwa mshambuliaji Mnyarwanda Jacques Tuyisenge aliipatia Gor Mahia golo la pili kwa shuti la mbali baada ya kuanzishiwa mpira na kiungo Mkenya, Francis Kahata mpira wa adhabu ndogo.
Katika mchezo uliochezeshwa na marefa kutoka Mauritius Ahmad Imtehaz Heeralall aliyepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Cauvelet Louis Ralph Fabien na Akhtar Nawaz Rossaye, Gor Mahia ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusaka goli na katila dakika ya 59, Kiungo Deus Kaseke anafanikiwa kupata goli la kwanza akiwa anaacheza mechi yake ya kwanza tangu arejee kutoka Singida United alipodumu kwa msimu mmoja.
Gor Mahia wakaimarisha uongozi wao kwa bao la tatu lililofungwa na Nahodha Harun Shakava dakika ya 64, kabla ya kiungo Raphael Daudi kuifungia Yanga bao la pili dakika ya 81.
Yanga wataikaribisha USM Alger Agosti 19 kabla ya kwenda kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na wenyeji, Rayon Sport Agosti 28, mwaka huu mjini Kigali, Rwanda.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Youthe Rostand/Benno Kakolanya dk77, Juma Abdul, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pius Buswita, Yussuf Mhilu/Juma Mahadhi dk54, Papy Kabamba Tshishimbi, Matheo Anthony, Raphael Daudi na Deus Kaseke/Ibrahim Ajib dk61.
Gor Mahia: Boniface Oluoch, Humphrey Mieno, Philemon Otiemo, George Odhiambo/Bernard Ondiek dk90, Haron Shakava, Joash Onyango, Kevin Omondi/Lawrence Juma dk63, Jacques Tuyisenge/Charles Momanyi dk83, Francis Kahata, Samuel Onyango na Godfrey Walusimbi.
Kikosi
cha Yanga kilichoanza katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani
Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na
ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini
Dar es Salaam.
Kikosi
cha Gor Mahia kilichoanza katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani
Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na
ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini
Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Yanga Juma Mahadhi akiondoka na mpira katika mchezo wa kombe la
Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor
Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kiungo
wa Yanga Deus Kaseke akijaribu kumtoka mchezaji wa Gor Mahia katika
mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia
uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika
Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mashabiki
wa Gor Mahia wakifuatilia mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika
kati ya Yanga na Gor Mahia uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam.Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea wakati wa mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment