HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 13 July 2018

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAONYESHO SABASABA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwasili katika viwanja vya sabasaba yalikofanyika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Barbas Mwakalukwa alipotembelea Banda la Polisi katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza  Askari wa Usalama Barabarani Faustina Ndunguru akitoa maelezo juu ya usalama barabarani na matumizi ya alama za barabarani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimuuliza swali kwa kutumia mfano wa picha za magari Askari wa Usalama Barabarani Faustina Ndunguru kuhusu makosa ya kuvunja sheria barabarani. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Sajent Miriam  kuhusu jinsi Polisi Jamii wanavyofanya kazi kuhudumia wananchi. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba yanakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Konstebo wa Polisi, Jovin John kuhusu mbwa wa polisi wanavyoweza kusaidia katika kukamata wahalifu nchini. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba kunakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Inspecta wa Polisi Alex Chandi aliyekuwa akitoa maelezo kuhusu namna gani Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) hufanya kazi kukabili wanaoleta ghasia. Wa kwanza kulia ni Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Barbas Mwakalukwa. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba kunakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi, alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Inspekta  Polisi John Mabonda  wa Polisi kitengo cha malalamiko jinsi wanavyohudumia wananchi wenye uhitaji wa huduma yao. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba kunakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
(Picha na Mambo ya Ndani)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad