Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako, amekabidhi hundi ya Sh. bilioni 3.8 kwa ajili ya utoaji wa ruzuku kwa vyuo vilivyopo kwenye mradi wa kuendeleza ujuzi (SDF).
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kuzindua Mfuko huo wa kuendeleza ujuzi, uliofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali, Profesa Ndalichako, alisema lengo ni kuziwezesha taasisi zinazotoa mafunzo ya ufundi katika ngazi mbalimbali.
“Serikali inategemea kuwa fedha hizi zitatumika vizuri na kuwanufaisha watanzania wa kawaida, hasa wale wa vijijini, kupitia mafunzo haya ya ufundi na wataweza kupata stadi stahiki zitakazo wawezesha kupambana na mazingira yao,” alisema Profesa Ndalichako.
Alisema katika kutekeleza azma hiyo, wizara imeipa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tea), jukumu lakusimamia kipengele muhimu ndani ya huo cha Mfuko wa Maendeleo ya Ujuzi.
Profesa Ndalichako alisema, Kupitia mfuko huo Tea watakuwa na jukumu la utambua taasisi ambazo zina uwezo wa kutoa mafunzo kwa sekta za kimkakati na kuziwezesha kutoa mafunzo hayo kwa vijana wa kitanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na shughuli za kutoa huduma.
Amesema anatarajia kuwa kupitia mfuko huo wizara itafikia malengo ya kuhakikisha kuwa mchango wa sekta binafsi katika kudahili wanafunzi wa vyuo vya ufundi ngazi ya kati unaongezeka kutoka asilimia 21 ya mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 25 mwaka wa 2020.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Elimu Tanzania Dk Erasmus kipesha amesema TEA ina mamlaka kusimamia majukumu sita .
Aliyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kufadhili miradi ya Elimu katika ngazi zote ili kuinua viwango cha ubora wa Elimu na upatikanaji wake kwa usawa kulingana na mipango na Sera za kitaifa kwa lengo LA kukidhi mAhitaji kijamii.
Kuishauri serikali juu ya vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya mfuko wa Elimu na kutafut rasilimali kwa ajili mfuko wa Elimu ikiwa ni rasilimali fedha au vifaa pamoja na Kutayarisha na kitathmn Mara kwa Mara vigezo na taratibu za kutenga na kutoa fedha za mfuko wa Elimu kwa Ngazi zote nchini.
Kufustilia na kuhakiki matumizi ya fedha za mfuko zilizotolewa kwa bodi mikopo,kamisheni ya vyuo vikuu na baraza la Elimu ya ufundi.pamoja mj na kujenga ushirikiano na na taasisi za ndani na nje nchi kwa lengo kuboresha elimu.
Pia amesema mamlaka imeshiriki katika hatua mbalimbali za uanzishwsji wa mfuko wa sdf unaenda sambamba na dira ya taifa 2025 ya kuwa na jamii iliyoelinika vyema na inayojifunza
"Tunatambua kuwa ufanisi wa SDF utachangia sana utekelezaji wa ilani ya chama Katika kipindi 2015-2020 sekta za uzalishaji Mali kama kilimo,ufugAji,uvuvi,viwanda vikubwa na vidogo na huduma kiuchumi km vile miundombinu ya nishati ,uchukuzi na ujenzi zitaelekeza mipango yao ktk kupunguza umaskini na kuanziadha ajira hususan kwa vijana” amesema.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa Mfuko wa kuendeleza ujuzi, uliofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi wa TEA, Profesa Maurice Mbago akizungumza kuhusiana na utekelezaji wa fedha hizo katika kuendeleza ujunzi katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi Mfano wa Hundi kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya utoaji wa ruzuku kwa vyuo vilivyopo kwenye mradi wa kuendeleza ujuzi (SDF).
Baadhi ya wakuu wa vyuo na watendaji mamlaka za elimu zilizo chini ya Wizara ya Elimu.
Picha ya pamoja ya wakuu wa vyuo na watendaji mamlaka za elimu zilizo chini ya Wizara ya Elimu.
No comments:
Post a Comment