HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 13, 2018

URAFIKI KATI YA CCM NA CPC WALETA MKUTANO WA HADHI YA KIDUNIA DAR

*Utafanyika kuanzia Julai 17 hadi Julai 18 mwaka huu, Rais Magufuli kutoa neno

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
UKWELI ni kwamba macho na masikio ya nchi mbalimbali barani Afrika na nchi nyingine duniani yatajikita nchini Tanzania kuanzia Julai 17 hadi 18 mwaka huu.

Unajua kwa nini?Ni kwasababu kutafanyika mkutano wa vyama vya siasa wenye hadhi ya dunia na Tanzania imepata nafasi ya kuandaa mkutano huo ambao umeratibiwa na Chama cha Kikomunisti cha China(CPC).

Ni mkutano unaolenga kujadili mambo mbalimbali na hasa mchango wa vyama vya ukombozi barani Afrika sasa kuweka mikakati ya kujenga uchumi imara kwa nchi za Afrika.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole ni akizungumzia ujio wa mkutano huo amesema utahudhuria na na zaidi ya watu 138 kutoka nchi mbalimbali zikiwamo za nje ya Bara la Afrika na vyama zaidi ya 30 vitashiriki.

Kwa mujibu wa Polepole waadau mbalimbali wakiwamo viongozi mashuhuri, wanasiasa wakongwe na watu maarufu watashiriki na kutoa mchango wao kwa maslahi ya vyama hivyo na Bara la Afrika kwa ujumla.

"Tanzania inatarajia kupokea ugeni mkubwa wa viongozi ambao watakuja kushiriki kwenye mkutano huo wa kidunia,"amesema Polepole wakati anazungumzia mkutano huo.

Kwanini mkutano huo unafanyika Tanzania? Majibu yanaweza kuwa mengi kulingana na mhusika atakavyoona inafaa.

Lakini ukweli ni kwamba mkutano huo unafanyika nchini kutokana na utulivu, amani , upendo na mshikamano na kubwa zaidi ni urafiki wa kidugu na wa damu wa muda mrefu kati yetu na nchi ya China.

Kwa kukumbusha tu kabla ya mkutano huo kuamriwa kufanyika Tanzania kuna nchi nyingi nazo zilitamani mkutano huo ufanyike kwenye nchi zao na moja ya nchi hizo ni Afrika Kusini.

Baada ya CPC kupima na kuchuja wakaona eneo ambalo ni sahihi kuufanyika mkutano huo ni Tanzania na ikumbwe ni mkutano wa kwanza mkubwa wa China kufanyika nje ya nchi yao.
Nieleze japo kidogo umahiri, uhodari na uchapa kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli umechangia kwa kiasi kikubwa China kuamua mkutano huo ufanyike nchini.

Hivyo kabla ya kuendelea nitumie fursa hii kutoa pongezi na shukrani kwa Rais Magufuli kwa utendaji kazi wake ambao umewakuwa ukiwafurahisha mataifa makubwa mbalimbali duniani likiwamo Taifa la China.

Pamoja na yote iko hivi nia ya CPC ya kuhakikisha kunafanyika mkutano huo ni kuangalia namna ambavyo watajadiliana na viongozi wa vyama vya ukombozi katika kusukuma maendeleo ya Afrika mbele.

Kwa Tanzania ni fahari kubwa mkutano huo kufanyika nchini kwetu kwani pamoja na mambo mengine itakuwa fursa ya kujifunza na kupata uzoefu wa mambo mbalimbali yakiwamo ya teknolojia na  uchumi.

China kupitia viongozi wake mahiri na wenye kuheshimika duniani ambao wanatokana na CPC wamekuwa mfano wa kuigwa katika maendeleo ya kukua kiuchimi na kulifanya Taifa hilo ndani ya miaka 73 limepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Hivyo uzoefu wa CPC kwenye mkutano huo utakuwa chachue kubwa inayoweza kuifanya Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali.

 Ni ukweli usiopingika Tanzania imetoa mchango mkubwa katika kusaidia ukombozi wa nchini mbalimbali za Kusini mwa Afrika.Mchango ambao unakumbukwa na mataifa mbalimbali na China ikiwa miongoni mwao.

Hata hivyo wakati ukitarajiwa kufanyika kwa mkutano huo mkubwa nchini kwetu kuna mambo kadhaa ambayo Watanzania lazima tukubali na huenda ikawa chachu ya China kuona mahala saahihi ya kufanyika kwa mkutano huo ni kwetu.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dk.Magufuli kuna mambo mengi ambayo anafanya katika uongozi wake yanaivutia China .Rais Magufuli tangu aingie madarakani ametoa msimamo wa Serikali katika kuchukia na kukomesha rushwa.

Amejenga uwajibika sehemu za kazi na moja ya jambo ambalo analifanya ni namna ambavyo amedhamiria kuleta maendeleo ya Watanzania na katika hilo ameamua kuweka kauli mbiu yake ya Hapa Kazi Tu.

Sote pia tunafahamu urafiki wa miaka mingi wa muasisi wa Taifa la Tanzania Mwalim Julius Nyerere pamoja na muasisi wa Taifa la China Mao Setung.Urafiki wa viongozi hao ulipanda mbegu inayochipua vizazi na vizazi.

Mbegu ambayo imeifanya China na Tanzania kuendelea kushirikiana na kushikamana katika kufanya maendeleo.Ni ukweli wa dhahiri China inaona Tanzania kuwa ni zaidi ya rafiki na wameendelea kuwa wamoja siku hadi siku.

Kuna miradi mingi ambayo inafanyika nchini kwetu kutokana na urafiki kati ya nchi hizo mbili.Hakika China ni Tanzania na Tanzania ni China.

URAFIKI WA CHINA, TANZANIA

Urafiki kati ya Tanzania na China unaweza kuelezea katika mitazamo tofauti lakini kwa lugha rahisi China imekuwa rafiki wa kweli kwa nchi yetu na Bara la Afrika kwa ujumla.

China ndiye mshirika atakayefanikisha kufikiwa mafanikio ya kweli ikiwa nchi hizo zitaiga kwa vitendo njia ilizopitia China katika kufikia mafanikio ya sasa.

Akizungumza katika mkutano wa kidunia wa vyama siasa ulioandaliwa na CPC Mjini Beijing Desemba Mosi, mwaka jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Rais Xi Jinping, alieleza bayana ni kwa jinsi gani nchi yake imekusudia kusaidia upatikanaji wa ustawi wa jamii katika nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Xi, alisema China imeweza kupiga hatua na kufikia ilipo sasa kutokana na mambo mengi ikiwemo kuwajibika na kusimamia utamaduni wake.

“Kwa utamaduni wetu sisi China tunaamini binadamu wote duniani ni ndugu. Tunaamini kila mmoja anaweza kupiga hatua kama akitaka kufikia mafanikio, jambo la msingi na muhimu ni kuwajibika,”alisema.

Hata hivyo, alisema maendeleo ya teknolojia yametengeza tofauti kubwa ya kiuchumi na umasikini kati ya nchi za Kusini na Kaskazi kutokana na tofauti ya kimtazamo.

“Mtazamo wa mwenye nguvu ndiye mwenye haki ya kuchukua chote unaweza kutekeleza maendeleo ya upande mmoja na kuviza maendeleo ya mwanadamu,”anasema.

“Lazima tufanye kazi kwa manufaa ya wote na kuhamasisha  uchumi wenye manufaa kwa wote katika mazingira ya ukweli na uwazi ambao utachochea mafanikio na maendeleo ya binadamu.

“Endapo hilo litafanyika litasaidia nchi mbalimbali kuwa na mwendo sawa wa kufikia maendeleo, kuondoa umasikini na kuhakikisha watoto wanahudumiwa ipasavyo,”alisema.

Hata hivyo unapofuatilia hotuba za Rais wa China kwa sehemu kubwa unaweza kubaini kuna mambo ambayo anajifunza kutoka Tanzania na hasa kupitia Rais Magufuli ambaye kimsingi anachotaka ni kuona Tanzania inafanikiwa tena ikiwezekana katika kipindi kifupi kijacho.

Na hiyo inaweza kutokana na ukweli kwamba misimamo ya Rais katika maendeleo ya Taifa yake iko dhahiri na hivi sasa wakati mkutano huo ukitarajiwa kufanyika nchini kwetu huenda wakapata nafasi ya kuelezwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM.

CHINA NI RAFIKI WA KIHISTORIA
China imekuwa rafiki wa kihistoria kwa Tanzania tangu enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya Kwanza chini hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Tangu awali nchi hiyo kupitia CPC ambayo ni rafiki wa karibu wa Cgma Chama Mapinduzi (CCM) ilionyesha dhamira ya dhati ya kuwa rafiki anayetaka kuona Tanzania na Afrika ikipata manufaa baada ya kukubali kutoa mkopo na kusaidia ujenzi wa Reli ya TAZARA.

Ambapo tangu ilipoanza kutumika hadi leo imekuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio ya kiuchumi.

Kabla ya China kukubali kujenga reli hiyo, ziliombwa baadhi ya nchi kubwa zenye maendeleo ya kiuchumi lakini zilikataa kuikopesha Tanzania na kufanikisha ujenzi wa reli hiyo.

Hatua ya China kukubali kujenga TAZARA ambayo sasa situ imekuwa kiunganishi cha mawasiliano katika ya Tanzania na Zambia, bali imekuwa pia ikitumika kusafirisha watalii na maelfu ya tani za mizigo.

kwa mazingira ya aina hiyo utabaini namna ambavyo China inaina Tanzania kama nchi pekee ambayo imekuwa na urafiki wa udugu ambao umejikita katika kusaidiana zaidi kwa maslahi ya wananchi wa pande zote na si urafiki wa mashaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad