HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 30 July 2018

TFF WAMESAINI MKATABA NA KCB KUDHAMINI LIGI KUU MSIMU HUU

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia wakikabidhiana mkataba baada ya kusaini Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420 katika hoteli ya Serena leo jijini Dar es salaam kulia ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420 kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chilo baada ya kusaini mkataba wa udhamini kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCM Bi. Fatma Chilo wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa KCB Bank na TFF.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya watendaji wa benki ya KCB wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio katika mkutano huo.

Na khadija Seif ,Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 420 na Benki ya KCBenwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu Benki ya KCB  nchini Cosmas Kimario ameeleza madhumuni ya Benki hiyo ni kushirikiana na TFF kwa ajili ya kukuza sekta ya Michezo ambapo walishashirikiana kwenye msimu  uliopita 2017/2018  kwa kuwa moja wa wadhamini wa ligi kuu nchini.

Kimario amesema udhamini huo unalenga zaidi kuendeleza soka hilo nchini pamoja na kuwapatia ajira  vijana na kuipeperusha bendera ya nchi ya Tanzania.

Rais wa  shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF)  Wallace Karia ametoa shukrani za dhati kwa bank ya KCB kwa udhamini huo kwani watanufaika na kusaidia kunyanyua michezo  kwenye msimu 2018/19.

Licha ya hiyo , Karia amesema Benki ya KCB imekuwa ikishirikiana na TFF kwenye michezo na hata msimu uliopita walishirikiana nao kudhamini michezo nchini na hii ikiwa ni mara ya pilo.

Kaimu mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Fatma Chiro ambapo ameeleza Benki hiyo imetoa ajira kwa watu wengi na rasmi inaunga mkono kauli ya serikali katika kutoa ajira kwa vijana na wameamua kuanza na sekta ya michezo.

Amefafanua zaidi kuwa benki hiyo haitaishia hapo kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu (TFF) katika kudhamini michezo hususani mpira wa miguu na kutazama uwezekano wa kusaidia timu ya mpira wa miguu ya wanawake Kilimanjaro Queens ambao wameshinda mechi waliocheza hivi karibuni dhidi ya Ethiopia na kurudi na kombe nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad