HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 23 July 2018

Puma Energy Tanzania yakabidhi gawio la bilioni 18 kwa wanahisa wake

Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania leo imekabidhi kwa Rais John Pombe Magufuli gawio la sh bilioni 9 kwa Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 kwa mwaka 2017 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Puma Investments Limited. 

Kampuni hiyo inamilikiwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50 na hivyo kupitia gawio hilo kila mwanahisa amepata shilingi bilioni tisa (9).

Akizungumza,kwa niaba Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Limited Philippe Corsaletti, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck Hiliyai alisema kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 100% ikilinganishwa na gawio la mwaka 2015 na kwa asilimia 29% ikilinganishwa na gawio na mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Hiliyai, kufikia mwisho wa mwaka jana kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi 31 bilioni huku ikiwekeza takribani shilingi 9 bilioni kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo kununua vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni juhudi za kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

“Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,’’ alisema.

Alisema ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2017 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato. “Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko.’’

Kwa mujibu wa taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12% mwaka 2015 hadi asilimia 14% kwa mwaka 2017.

Bw Hiliyai amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt John Pombe Magufuli kwa mikakati yake ya kukusanya kodi na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2017/2018.

“Mikakati hii imeweza kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi. Mazingira haya mazuri ya biashara yameiwezesha kampuni ya Puma kukua zaidi kutoa gawio mara mbili zaidi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.,’’ alisema

Aliahidi kuwa kampuni hiyo itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa.Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege. 
 Rais John Pombe Magufuli  (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) na Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia)
 Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa kwa Rais John Pombe Magufuli  (katikati) ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited. Hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija. Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango wakati wa hafla ya makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad