HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 24, 2018

MAHAKAMA YA TANZANIA YASEMA HAINA SABABU YA KUGOMBANA NA TLS

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Mahakama ya Tanzania imesema haina sababu ya kugombana na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kwani mahakama haiwezi kuishi bila mawakili na wao hawawezi kuishi bila  mahakama. 
Msajili Mkuu wa Mahakama, Catherine Revocati ameyasema hayo wakati 
Uongozi wa TLS chini ya Rais wake, Fatuma Karume ulipokutana na Jaji Mkuu leo Julai 24, 2018 kukubaliana  kushirikiana katika mabadiliko ya Tehama.

Msajili Revocati amesema,  mahakama ipo katika dira ya Mpango Mkakati wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambayo inahusisha wadau wote wa mahakama.

Amesema hatua hiyo inalenga kuondokana na mfumo wa kutumia makaratasi, ambapo mabadiliko hayo yanapaswa kuhusisha wadau wote wa kisheria ikiwemo TLS. 

Ameongeza kuwa, wameona ni vema wakashirikiana na TLS hasa katika upande wa Tehama, kwani hawana sababu ya kugombana maana Mahakama haiwezi kuishi bila Mawakili na hata wao mawakili hamuwezi kuishi bila mahakama,

Aidha, Revocati amewaomba mawakili  waendelee kujiandikisha katika mfumo huo mpya ili kuendana na mabadiliko hayo.

Kwa upande wake, Rais wa TLS, Fatuma Karume amesema mabadiliko hayo ni mazuri na yatasaidia kuweka uwazi katika jamii hasa kwa kujua taarifa zozote kuhusu mahakama zikiwemo taarifa za hukumu. 

"Kama hukumu ikitoka na ikawepo kupitia mitandao nadhani watu watakuwa na fursa ya kuhoji kama hukumu imekosewa ama la,  mahakama haiwezi kuboresha mazingira ya utoaji haki katika maamuzi kama hawatashirikiana na TLS kwa sababu wao ndio watu wanaokutana na watu wenye kesi.
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati akimkaribisha Rais wa TLS pamoja na Viongozi wengine TLS alioambatana nao alipotembelea Mahakama ya Rufani mapema Julai 24.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma akiongea jambo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),  Fatma Karume pindi Rais huyo pamoja na Viongozi wengine wa Chama hicho walipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam mapema Julai 24, 2018.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Fatma Karume (katikati) na viongozi wengine wa Chama hicho.
Rais wa TLS na Viongozi alioambatana nao wakifuatilia kwa makini mada kuhusu Mpango Mkakati na Maboresho ya Mahakama ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maboresho-Mahakama, Bw. Sebastian Lacha.
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania,  Katarina Revocati akifafanua jambo, kushoto ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),  Fatma Karume.
Rais wa TLS akifurahia zawadi ya nakala ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama ya Tanzania aliozawadiwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume akitoa neno la shukrani mara baada ya majadiliano katika ya TLS na Mahakama, katika majadiliano Viongozi hao wameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano, katikati ni Msajili Mahakama ya Tanzania,  Katarina Revocati na kulia ni Mtendaji, Mahakama ya Rufani (T), Bw. Solanus Nyimbi.(Picha na Mahakama)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad