HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 19 July 2018

MAHAKAMA MORO YAZUIA WATUHUMIWA WANAOACHIWA KUKAMATWA NDANI YA VIUNGA VYA MAHAKAMA HIYO

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro, imezuia watuhumiwa wanaoachiwa kwa kifungu ambacho kinaruhusu wao kukamata, kukamatiwa ndani ya viunga vya mahakama hiyo.

Hayo yameelezwa leo mkoani hapa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro Elizabethi Nyembele wakati wa ziara ya waandishi wa habari za mahakamani walipofika katika Mahakama hiyo.

Waandishi hao wapo katika mafunzo ya siku tano yambayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.Mafunzo hayo yameahirikisha waandishi 30 wa vyombo mbalimbali nchini.

Amesema, wamezungumza na Polisi wasiwakamate watuhumiwa pindi wanapokuwa wameachiwa ndani ya viwanja vya Mahakama kwani ni fedhea.

" Tumezungumza na Polisi wasifanye hivyo, kwa sababu mara nyingine mshtakiwa anakamamatwa hata mbele ya hakimu bila kujali wapo katika eneo gani,

" Mtuhumiwa anakufuata anakwambia mheshimiwa naomba nilinde wanataka kunikamata kitendo ambacho si kizuri na hakileti picha," amesema Hakimu Nyembele

Ameongeza kuwa, hakimu anapoifuta kesi huku akijua inahitilafu kisheria anamueleza mtuhumiwa kuwa anaweza kufunguliwa kesi nyingine.Wengine ni waelewa unamuachia pale pale anaingia mikono ni mwa polisi bila kukimbia

" Zamani watu wamefariki kwa sababu ya hiyo hiyo ya kukimbia, anaweza kuwa ameachiwa ile furaha akakimbia, mwingine hajui kama ameachiwa na ameona amemtoa Magereza atampiga risasi kwa sababu anajua ametoroka, huwa tunawapa elimu wasifanye hivyo," amesema.

Aidha, ameeleza kesi za unyang'anyi, dawa za kulevya na kesi za ujangili ndizo zinazoongoza katika Mahakama hiyo na hiyo inasababishwa na mkoa kuzungukwa na mbuga na mapori

Pia amesema Mahakama hiyo imepiga hatua katika suala la rushwa, kutokana na elimu wanayowapatia watumishi na pia wamebandika matangazo mengi kuwa huduma zote ni bure kwa lengo la kuepusha rushwa.

Kwa upande wake Mtendaji wa mahakama hiyo, Nestory Mujunangoma amesema wanachangamoto ya vyumba vya mahakama, lakini hivi sasa wapo kwenye ujenzi wa jengo la ghorofa nne ambalo litakuwa na huduma zote,kuanzia Mahakama zote hadi vyumba vya rufaa.

Hakimu Mkazi  Mwandamizi  Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Elizabeth Nyembele akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotembelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye moja ya ziara za kimafunzo kwa Waandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  Elizabeth Nyembele akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri kuanza kwa mashauri yao kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro katika ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari  mkoani Morogoro.  (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOROGORO)
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  Elizabeth Nyembele akionyesha waandishi wa habari nembo ya iliyopo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele hayupo kwenye picha.
Mtendaji wa Mahakama mkoa wa Morogoro Nestory Mjunangoma akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanahabari wakiendelea na ziara yao
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akimsikiliza mmoja wa waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo ya kimafunzo kwa waandishi hao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad