HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 19 July 2018

MAAFISA UHAMIAJI WAANZA KUNOLEWA KATIKA MAFUNZO YA WADAU KATIKA MNYORORO WA UTALII

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
CHUO KIKUU cha utalii kinachotoa huduma ya utalii, ukarimu na utafiti kimeandaa kozi fupi kwa wadau muhimu katika mnyororo wa utalii wakianza na maafisa uhamiaji ili kuweza kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii ambapo Chuo hicho kilicho chini ya Wizara ya Utalii na Maliasili, sekta ya utalii ni moja kati ya sekta ambayo huiingizia kipato serikali.

Akizungumza na vyombo vya habari Ofisa Mtendaji Mkuu Chuo Kikuu cha Utali Shogo Sedoyeka ameeleza kuwa dhima ya kuandaa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na watalii milioni 2 ifikapo 2020.

Ameeleza kuwa nguvu za ziada zinahitajika ili kuweza kuyafikia malengo kwa kuwa sekta hiyo  mtambuka inashirikiana na sekta nyingi kama afya na miundombinu huduma ambazo watalii huhitaji wakiwa nchini.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wadau muhimu kama vile maafisa uhamiaji, polisi na usafirishaji na wadau wengine ili kuweza kufikia malengo na wameanza na maafisa uhamiaji.

Kuhusu mafunzo hayo Shogo ameeleza kuwa yatahusu mada mbalimbali kama vile: huduma kwa wateja, mapokezi, mbinu za kushughulikia malalamiko ya wateja, muda katika utoaji wa huduma, mawasiliano na wateja na jinsi ya kuhudumia wateja wenye mahitaji maalumu.

Amewataka maafisa wahamiaji kuzingatia mafunzo hayo ambayo mbali na kuongeza kipato kwa taifa wataitangaza nchi na  kupata watalii wengi zaidi kutokana na huduma bora zitakazotolewa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka(kulia) akifungua mafunzo ya  kuwajengea uwezo kwa maafisa uhamiaji ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na watalii milioni 2 ifikapo 2020 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam. 

 Baadhi ya maafisa uhamiaji wakisikiliza hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka alipokuwa anafungua mafunzo kwa maafisa hao kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam leo.
Mkufunzi Jesca William akitoa mafunzo kwa maafisa uhamiaji kuhusu umuhimu wa wageni pamoja na sifa za mtoa huduma wakati wa mafuzo yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam.
Mafunzo yakiendelea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad