HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 30 July 2018

LTSP YAPONGEZWA KWA KUTATUA KERO ZA ARDHI MOROGORO

Mradi wa kuwezesha umilikishaji wa ardhi LTSP, umepongezwa kwa kufanikiwa kutatua kero ya migogoro sugu thelathini na tano ya ardhi iliyodumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na tano  na kusababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali.

Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Charles Kabeho wakati wa zoezi la ugawaji wa hati 3,063 za kimila kwa  wanavijiji wa vijiji vya Igima na Mpofu vilivyoko kata ya Mbingu,wilaya ya Kilombero mkoani morogoro.

“Napenda kuishukuru serikali kupitia mradi wa upimaji na urasimishaji ardhi(LTSP) chini ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutatua migogoro hiyo kwa kupima ardhi,kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi na utoaji wa hati za kimila,”alisema.

Aliongeza tangu mradi huo wa majaribio ufike kwenye wilaya tatu za Malinyi,Ulanga and Kilombero,migogoro hiyo imekomeshwa kwa kufanya uratibu mzuri wa masuala ya ardhi.
                                                                  
Kwa mujibu wa kiongozi huyo,hati hizo za kimila zitawasaidia wanavijiji hao kupata mikopo na kuhuisha thamani ya ardhi zao tofauti ilivyo awapo awali.

Aliongeza kuwa migogoro ya ardhi mkoa humo ilileta changamaoto kubwa kwa serikali na wakazi hao ikiwemo hofu hali iliyorudisha nyuma uzalishaji na hivyo kurudisha nyuma  maendeleo yao.

Akisoma taarifa fupi ya Mradi wa Urasimishaji,Mratibu wa Mradi huo,
Godfrey Machabe alisema kuwa mradi huo unatekelezwa baina ya serikali na Mashirika ya Maendeleo ya Denmark(DANIDA),Swedeni (SIDA)  na Uingereza(DFID) na kusema kuwa mradi utakapokwisha mwakani uzoefu uliopatikana utatumika kwenye mikoa mingine.

Alisema mradi huo umetumia jumla ya shilingi billioni  78.3 kwa ajili ya  upimaji  wa mipaka ya vijiji vya Igima na Mpofu, mipango ya matumizi ya ardhi, uandaaji wa mipango ya kina ya ardhi pamoja na kuandaa hati miliki za kimila. 

Aliongeza kuwa kwa upande wa Igima jumla ya viwanja 2701 vimefanyiwa utafiti katika kijiji cha Igima na viwanja 3063 vimefanyiwa utafiti katika kijiji cha Mpofu.

Akitolea mfano wilaya ya Kilombero, Machabe alisema kuwa kwa mfano, kulikuwa na viwanja 43, Ulanga (40) na Malinyi (22) wakati huo huo mradi huo ulikuwa umeandaa Hati ya Kikabila ya ardhi ya kijiji (CVL)

Akielezea mafanikio makuu yaliyopatikana na programu hadi sasa, alisema mradi huo umeweza kutatua migogoro zaidi ya thelathini mikubwa ya ardhi iliyodumu kwa zaidi ya miaka kumi na tano mkoani humo.

Alisema kati ya migogoro hiyo, (35)  wilaya ya Kilombero ilikuwa na (12), Ulanga (12) na (11), wilayani Malinyi na kuongeza kuwa mpango huo uliweza kutatua mipaka ya ardhi ya vijiji nane wilayani kilombero Kilombero, kumi na moja huko Ulanga na nne katika wilaya ya Malinyi.

“Ni matumaini yangu kwamba mara tu mpango huo utakapokuwa mwishoni mwa Juni 2019, uzoefu uliopatikana kutoka kwa mradi utaongezwa kwa halmashauri nyingine za wilaya nchini," alisema Machabe.
 Mratibu wa mradi wa Mradi wa LTSP Godfrey Machabe akisoma taarifa ya mradi kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Mabeho (Hayupo pichani) baada ya Mwenge kuwasili katika kijiji cha Igima Kata ya Mbingu Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Mabeho akimkabidhi Hati ya Kimila mkazi wa kijiji cha Igima katika hafla fupi iliyofanyika mara baada ya Mwenge kuwasili kijijini hapo. 
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Mabeho akipata maelezo kutoka kwa kiongozi wa kazi za uwandani wa mradi wa LTSP Swagile Msananga baada ya Mabeho kufika katika banda la LTSP 
Charles Mabeho akiwa na viongozi wa wilaya ya Kilombero, Mratibu wa mradi wa LTSP na wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge wakicheza muziki uliokuwa ukiimbwa na Mrisho Mpoto (hayupo Pichani)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad