HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 31 July 2018

DC MJEMA AFUNGUA BARAZA LA UVCCM ILALA, APONGEZWA KUSHIRIKISHA VIJANA MBIO ZA MWENGE

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefungua baraza la umoja wa vijana (UVCCM) katika kata zote za Ilala na kujadili masuala ya kimaendeleo ya jimuiya na chama.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mjema ameeleza kuwa baraza hilo litaleta maendeleo kama ilivyokuwa kwa wanawake wa Wilaya hiyo hasa ya kimaendeleo.

Aidha amewahaidi vijana hao mabadiliko na kuwataka wakae mkao wa kula kwani Agosti mwaka huu vijana wote wa Ilala maisha yao yatabadilika katika shughuli za kijasiriamali ambazo kama Serikali imejizatiti kuwahudumia.

Pia amewashauri vijana hao kuwa na nidhamu ili kwenda mbele zaidi na wafuate kanuni, taratibu na sheria sambamba na mshikamano na upendo.

Mjema amewashukuru vijana hao kwa ushirikiano wanaoonesha katika shughuli za kijamii.

Naye Mbunge wa Ilala na mwenyekiti wa kamati za Bunge Idd Azan Zungu amewashauri vijana katika kuwekeza na kufanya kazi kwa bidii na watumie asilimia 40 ya fedha iliyotengwa kwa vijana kuleta maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Pia mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Ramadhan Mlawa amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kushirikisha vijana katika shughuli za kijamii hasa katika kukimbiza mwenge wa uhuru  mwaka huu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau na vijana kutoka kata za kitunda, Chanika na Mchafukoge.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad