Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), limejipanga kuondoa kero ya mivujo ya Maji
katika mitaa yote ya Wilaya Temeke ambayo imekuwa ikiripotiwa na wakazi pamoja na viongozi wa
serikali za mtaa katika wilaya hiyo.
Hayo yamebainshwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Temeke Bw. Xavery Ndondole katika kikao
chake na viongozi wa serikali za mitaa cha kujadili huduma ya Maji katika wilaya hiyo ambapo
ameeleza kwamba mivujo mingi inatokana na miundombinu chakavu inayoshindwa kuhimili msukumo
wa Maji yaliyoongezeka katika maeneo mengi.
“Maji ni huduma ya msingi na hayana mbadala ni lazima tuzuie upotevu wa Maji ili wananchi wengine
wasioyapata wapate kuyatumia hivyo nawaomba tushirikiane kwa kutoa taarifa muda wowote pale
unapokutana na mivujo ya aina yoyote katika eneo lako na sisi Dawasco tutafika fika na mafundi wetu
kwa wakati” alisema Ndondole
Hata hivyo mwenyekiti wa Kata ya Keko Bw. Shilingi S. Shilingi ameeleza kuwa kumekuwa na tabia ya
baadhi ya Mafundi kutoka Dawasco kufanyia ukarabati mivujo mikubwa peke yake na kupuuzia taarifa
za mivujo midogo midogo katika mitaa nakulekea madimbwi na mitaro kujaa.
“Mivujo imekuwa kero na hata gari zenu zinapita huko mitaani kwetu wanafika ila bado kuna
mabwawa, mivujo ni mingi ila mafundi wenu wanafanyia kazi mivujo mikubwa lakini midogo wanaacha
bila kufanya chochote nahii ndo mingi huko kwetu” alisema Shilingi.
Pia katika kikao hicho uongozi wa Dawasco Temeke umewaomba viongozi hao wa serikali za mitaa
kutoa ushirikiano kwa wananchi wanaohitaji huduma ya Maji kwa kuwapa fomu za utambulisho ili
waweze kuunganishiwa huduma ya Maji kwa wakati.
No comments:
Post a Comment