HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 20 June 2018

WAZIRI UMMY AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA MDEMU

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akiweka jiwe la msingi Mradi wa ukarabati na uboreshwaji katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma leo.kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mzee na Mbunge wa Bahi Bw. Omari Baduel.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua majengo ya wodi ya wajawazito,jengo la upasuaji wa dharura ,Mochwari ,sehemu ya kuchomea taka na maabara katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasalimia wanakijiji waliojitokeza  wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu kilichopo wilayani Bahi mkoa wa Dodoma .
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wanakijiji wa kata ya Mdemu hawapo pichani wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu wilayani Bahi  jijini Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Bahi Bw. Omari Baduel akiongea na wanakijiji wa kata ya Mdemu hawapo pichani wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu wilayani Bahi  jijini Dodoma, kushoto waliokaa ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi. Elizabeth Kitundu
 Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mafundi wakiwa katika hatua ya mwisho ya kumalizia jengo la Mochwari lilipo katika Kituo cha Afya Mdemu Wilayani Bahi Mkoa Dodoma. PICHA NA WIZARA YA AFYA -DODOMA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad