HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 June 2018

WALIMU WASTAAFU KUANZISHA SHULE YA MFANO SONGEA

 Walimu wastaafu katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kuanzisha shule ya Sekondari ya mfano katika manispaa hiyo.

Wakiongea kwenye kikao chao cha Taasisi ya walimu wastaafu Songea (TAWASO) walimu hao walisema kuwa ipo haja ya walimu kuanzisha shule ya mfano ambayo itamwandaa mwanafunzi kujikita katika kujitegemea baada ya kutegemea ajira za serikali.

Mwenyekiti wa Tasisi ya walimu Wastaafu Songea bwana Rashidi Maulidi Ngerangera alibainisha sababu ya kuanzisha shule ambayo itakuwa ya mfano na itawaandaa vijana katika maisha ya kujitegemea baada ya kutegemea ajira serikalini.
 Bwana Ngerangera alidai kuwa walimu hao wamedhamiria kuanzisha sekondari hiyo ambapo itachukua masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na masomo ya ufundi ili kumwezesha kijana amalizapo kidato cha nne aweze kwenda kujitegemea badala ya kusubiri ajira za serikali pekee.

Aidha katibu wa Taasisi hiyo bwana James Kaupunda aliwaambia wanachama wenzake kuwa ili waweze kufanikisha hilo ni lazima michango waliyokubaliana kwa kila mwaka ambayo ni 1,500,000 kwa kila mwanachama aweze kutolewa kwa wakati ili adhima yao ya kujenga sekondari hiyo iweze kukamilika .

Bwana kaupunda aliwasomea gharama ya ujenzi wa darasa lililojengwa na Taasisi hiyo kuwa limegharimu milioni 12 na ili kuweza kukamilisha uwekaji wa milango na madirisha nilazima wachangie kwa wakati na kazi ifanyike kwa wakati.
Hata hivyo kwa mwaka 2017 wanataasisi 9 walifanikiwa kuchangia milioni 1,500,000 kila mmoja na kupata 13,500,000 ambazo ziliweza kujenga darasa moja la Taasisi hiyo ya TAWASO.

Kwa mwaka huu 2018 taasisi hiyo imepanga kujenga darasa la pili kwa kutumia michango yao binafsi na wamejipanga kuanza kuandika maandiko kuweza kuomba wafadhili watakao wasaidia waweze kukamilisha wazo lao la kujenga shule hiyo.

Taasisi ya Wastaafu hao ilianza na walimu 3mwaka 2012 na sasa taasisi hiyo inajumla ya wanachama 9 na wameweza kujenga darasa moja katika eneo la Shule ya Tanga kwa Bubu na kumiliki zaidi ya ekari 100.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad