HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 21 June 2018

WAGONJWA 11 KATI YA 20 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita  inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India .

Wagonjwa hao wamefanyiwa upasuaji wa   kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement).

Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wanne kati yao wameruhusiwa kutoka  katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

Katika kambi hiyo iliyoanza tarehe 18 hadi tarehe 23 mwezi huu  inaenda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa madaktari wetu pamoja na wauguzi. Jumla ya wagonjwa 20  ambao ni watu wazima  wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India  Ali Ascar Beliranwalwa akivuna mshipa wa damu ndani ya kifua na kuunganisha kwenye misuli ya moyo ili kuuongezea moyo damu katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo ya siku sita inayofanywa na Hospitali hiyo kwa kushirikiana na  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Tangu kuanza kwa kambi hiyo jumla ya wagonjwa 11 kati ya  wagonjwa 20 waliopangwa kufanyiwa  upasuaji  wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na  kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement) wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. 
  Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa  kubadili milango ya moyo  (Valve Replacement) ambayo haipitishi damu vizuri kwenye moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa  20 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
 Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa  kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Kwa kipindi cha siku tatu tangu kuanza kwa kambi hiyo jumla ya wagonjwa  11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad