HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 18 June 2018

WAFANYAKAZI WA BENKI YA EXIM TANZANIA WACHANGIA DAMU

 Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama akimtoa damu mfanyakazi wa Exim Bank Patrick Masawe wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniani (World Blood Donors Day 2018). 
 Afisa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa Damu salama, Mariam Juma akimpima damu mfanyakazi wa Exim Bank Daniel Lukuba wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniania (World Blood Donors Day 2018). 

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim waitoa damu.

KUFIKIA 14 Juni, 2018 benki ya Exim Tanzania ilifikia kilele cha kampeni inayoenda kwa jina la "Kupata damu katika benki ya damu kesho, leo" ambayo imejikita kuwahamasisha wananchi kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu inayofanyika kila tarehe 14 Juni duniani kote.

Lengo kuu la kampeni hiyo ambayo iliendana sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” ni kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa. Kampeni hiyo inaonyesha kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashirki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mpango huu kila mwaka unalenga kukusanya damu kwa ajili ya benki ya taifa chini ya usimamizi wa Mpango wa Taifa wa uchangiaji damu nchini [NBTS].

Kampeni hii ilianza rasmi katika tawi la Exim mkoani Arusha tarehe 4 Juni na kuendelea katika mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza. Tukio kuu limefanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  wafanyakazi 200 , wateja na jamii chini ya kauli mbiu ya kimataifa: " “Jitoe kwa ajili ya mwingine. Changia damu." Kampeni hii inakumbusha jukumu la kila mtu kujitolea katika kuwasaidia wengine katika hali ya dharura kwa kutoa zawadi ya thamani ya damu. Pia inasisitiza juu ya ukweli kwamba ni muhimu kutoa damu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwepo na damu ya kutosha kabla ya dharura kujitokeza. Kampeni hii ni sehemu ya programu ya majukumu ya shirika la kijamii ya benki ya Exim Tanzania iitwayo, Exim Cares. 

Akizungumza kuhusiana na kampeni hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Exim Bank Tanzania  Bw. Jaffari Matundu, alisema huu ni mwaka wa nane toka benki hiyo ianzishe kampeni hii ya uchangishaji damu kwa ajili ya benki ya taifa. "Ni fahari kwetu kuwa benki ambayo inawajibika kijamii, imekuwa utamaduni wetu sio tu kuhamasisha, lakini pia kushiriki kikamilifu katika kuimarisha sekta ya afya nchini. Tunaamini kwamba kushiriki kwa kutoa damu mara kwa mara bila kukosa, tunashiriki kikamilifu katika kuchangia matayarisho ya dharura ya huduma za afya katika nchi yetu".

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii. Katika miaka iliyopita benki imechangia zaidi ya lita 300 za damu katika Benki ya damu taifa na mwaka huu wantarajia kuchangia zaidi ya lita 200. Katika maandalizi ya kampeni hii, benki ilijitolea kuhamasisha wafanyakazi wake, wateja na umma kupitia njia za mbalimbali za mawasiliano ya ndani ya benki na mitandao ya kijamii ili kuhakikisha ushiriki wa kiwango cha juu.

Afisa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa Damu Salama, Mariam Juma alitoa shukurani zake kwa benki ya Exim kwa mchango wake wa kila mwaka kwa benki ya Taifa ya damu na hasa kwa mwaka huu ambapo kampeni hii imeangukia katika mwezi wa Ramadhan kipindi ambacho uchangiaji wa damu kwa kawaida huwa chini. "Tanzania bado inakabiliwa na upungufu mkubwa katika Benki ya Taifa ya damu kutokana na ukusanyaji mdogo na pia kutokuwepo na elimu ya kutosha, hivyo basi ni lazima tuendelee kupambana kueneza elimu ya kuwa tunahitaji wachangiaji damu wa mara kwa mara," alisema.

Ili kuwepo na mahitaji ya damu ya kutosha katika benki ya taifa ya damu, mashirika yanahimizwa kuchukua hatua kama ya Benki ya Exim katika kuchangisha damu na kufanya hivyo mara kwa mara.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad