TIMU 49 ZAJIANDIKISHA KUSHIRIKI MSIMU MPYA WA MICHUANO YA SPRITE BBALL KINGS - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 18 June 2018

TIMU 49 ZAJIANDIKISHA KUSHIRIKI MSIMU MPYA WA MICHUANO YA SPRITE BBALL KINGS

Afisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko akizungumzia zoezi zima la usaili kwa zitakazoshiriki michuano ya Sprite BBall Kings msimu wa pili unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Juni.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu 49 kutoka Jijini Dar es Salaam zimefanikiwa kufanya usaili wa ushiriki wa michuano ya Sprite inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings msimu wa pili yalizinduliwa mapema wiki iliyopita na kuzitaka timu kufanya usaili siku ya Jumanosi  ikiwa ni zoezi la siku moja kwenye Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya zoezi la usaili kwa timu shiriki likiendelea Afisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko alisema kuwa zoezi limeenda vizuri na mwitikio umekuwa mkubwa sana na timu zilizoshiriki mwaka jana nazo ziliweza kujitokeza na kufanya usaili.

Basilisa amesema kuwa, michuano ya mwaka huu yatakuwa ya kuvutia zaidi kwani timu nyingi zimejipanga na zimejiandaa kwa ajili ya kuleta ushindani kwa msimu huu wa pili.

"Michuano ya mwaka huu yatakuwa na ushindano mkubwa sana kwani timu zimejiandaa pamoja na zile zilizoweza kushiriki msimu wa kwanza wa Sprite BBall Kings ," amesema Basilisa.

"Kwa mwaka huu timu zimejipanga kuondoka na milioni 10 za ushindi na kombe, na Mchezaji bora wa michuano (MVP) ataondoka na Milioni 2 na kikombe ukiachilia mbali mshindi wa pili akijinyakulia Milioni 3," amesema.

Kwenye msimu wa kwanza wa Sprite BBall Kings timu ya Mchenga BBall Stars iliweza kuibuka na ubingwa wa Sprite BBall Kings 2017 akijinyakulia milioni 10 na kombe huku TMT wakishika nafasi ya pili na kujipatia milioni 3 huku mchezajj bora (MVP) Barongo akiondoka na milioni 2.

Baadhi ya timu zilizoweza kujiandikisha kwa msimu huu wa pili ni pamoja na Mchenga BBall Stars, TMT,Flying Dribblera, Ardhi University na Kurasini Heat ikija na jina jipya la Temeke Heroes baada ya kugawanyika kwa baadhi ya wachezaji wake.
Usaili wa washiriki wa Mashindano Sprite BBall Kings wakiendelea kujisajili kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kutimua vumbi Juni 23 mwaka huu uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mlimani City Mall , Jumla ya timu 49 ziliiweza kujisajili kwa ajili ya simu kwa msimu wa pili wa Sprite BBall Kings.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad