HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 22 June 2018

MWANAMKE AUAWA MANYARA, CHANZO CHA KIFO BADO HAKIJAFAHAMIKA, MMOJA ASHIKILIWA NA POLISI Inb


Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga

Na Vero Ignatus , Manyara.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jila la Josephine Peter (51)mkazi wa Mrara kata ya Mamire wilayani Babati ameuawa na watu wasiofahamika huku shingo yake ikikatwa na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza leo june 21 Kamanda wa polisi  mkoani Manyara  Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwanamke huyo alifariki dunia juni 19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake  na mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji hayo. 

Kamanda amesema kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi nakubainika  kuwa hajabakwa kama watu wanavyozusha  bali jeshi la polisi unaendelea na upelelezi wa tukio hilo la mauaji amesema kuwa ukikamilika taarifa kamili itatolewa 

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad