HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 15 June 2018

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA YAFANA WILAYA YA MKURANGA

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akimkabidhi  cheti Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake la uwezeshaji wa Kiuchumi Mariam Ulega  kama ishara ya shukrani kwa kusapoti Harakati mbalimbali za Maendeleo katika Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Filberto Sanga amewataka wazazi kuwajali na kuwapenda watoto wao kwani waliwaleta duniani kwa mapenzi yao wenyewe yawapasa kuwalea na kuwakinga na ukatili wa kijinisia.

Hayo aliyasema jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayofanyika kila mwaka na kwa Wilaya ya Mkuranga walifanya katika kijiji cha Magoza  Kata ya Kiparang'anda na watoto 108 wanaoshi kwenye mazingira magumu kuzawadiwa  zawadi mbalimbali.

Sanga amesema kuwa, wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha masomo watoto hao.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungunza na wanachi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika 

"Hakuna mtoto aliyeomba kuja duniani bali ni sisi wazazi kwa starehe zetu tumewaleta hawa watoto na lazima tuwajali na kuwalinda, kuwapa elimu na pia kutowakatisha masomo yao na kupelekea ndoa za utotoni," amesema Sanga.

Na kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake na mke wa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega amesema kuwa yeye pamoja na mumewe wameamua kusherehekea maadhimisho haya kwa kuwapatia watoto zawadi.

Mama Ulega amesema kuwa watoto ni tuni ya taifa yapaswa kulindwa kwani kauli mbiu ya mwaka huu katika siku ya mtoto wa Afrika kwa hapa nchini inayosema KATIKA UCHUMI WA VIWANDA WATOTO WASIACHWE NYUMA inalenga katika kuhamasisha watoto wasome kwa bidii ili baadae na wao waje kuwa wabunge na mawaziri.

Mama Ulega amesema, "Kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu, wazazi hawana budi kuwasisitiza watoto wasome kwa bidii ili baadae waje kuwa wabunge na mawaziri kama Ulega na cha zaidi ni kuwa watoto ni tunu ya taifa hili kuelekea uchumi wa viwanda," 

Pia, Mama Ulega alisema mbali na zawadi hizo kwa watoto pia Mh Ulega aliweza kutoa zawadi kwa watendaji wa kata na vijiji 36 kwa utendaji wao mzuri wa na kuwataka wasikatishwe tamaa na changamoto baadhi zinazojitokeza.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji wa Kiuchumi Mariam Ulega akitoa salumu za Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga wakati wa maadhimisho ya siki ya mtoto wa Afrika.

Mbali na Ulega kutoa zawadi hizo kwa pia Wabunge wa viti maalum mkoa wa Pwani Subira Mgalu, Zainab Vulu na Hawa Mchafu waliweza pia kuchangia  kiasi cha fedha na kufanikisha kupatikana kwa kilo 750 za mchele, sabuni na baadhi ua zawadi zingine walizopatiwa watoto hao ikiwemo doti 30 za kanga walizowapatiwa wazee wanaoishi na watoto yatika kutoka vijiji sita.

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka duniani kote na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zimekuwa zinajitolea kuhakikisha wanapigania haki za watoto na kutoa elimu zinazohusu umuhimu wa kuwapatia elimu watoto wote na kutowakatisha masomo na kuwaozesha.

Maadhimisho haya yalienda sambamba na kukabidhi misaada kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo vifaa vya shuleni na Bima za Afya kwa familia 150 zinazoishi katika Mazingira Magumu. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akimkabidhi  cheti Mkurugenzi wa Mwanamke na Uongozi Shamira Mshangama kamama ishara ya shukrani kwa kusapoti Harakati mbalimbali za Maendeleo katika Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akikabidhi cheti.


Matukio mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Mkuranga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad