HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 17 May 2018

WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MGANGA  Mkuu wa  Serikali  Profesa  Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inatambua umuhimu wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu katika kulinda ya afya ya wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ambapo amesema kikao cha baraza  ni kuhakikisha kuna kuwepo kwa uhusiano kati ya watendaji na Menejimenti.
Kambi amesema katika mkutano wa baraza wanatakiwa kujadili malengo ya taasisi na maslahi ya wafanyakazi ikiwemo mafunzo  ambayo yanatakiwa kutolewa kwa haki sawa.
Aidha Mganga Mkuu huyo ametaka wafanyakazi  wa (GCLA) kuachana na kuwa sehemu ya watu wanaolalamika badala yake wanatakiwa kutatua changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (GCLA), Dk. Fidelice  Mafumiko  amesema katika kikao  hicho watajadili mada mbalimbali ikiwa ni kuijenga  taasisi hiyo.
Dk. Mafumiko amesema pia baraza hilo kupitia kikao hicho wataazimia mambo mbalimbali yakiwamo ya kujenga mamlaka  ikiwa pamoja na masuala ya maadili.
 Mganga Mkuu wa Serikali,  Profesa Mohamed Kambi  akizungumza katika mkutano wa baraza la  wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu (GCLA) uliofanyika katika ukumbi wa MSD  jijini Dar es Salaam .
 Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu (GCLA), Dk. Fidelice Mafumiko akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA  kuhusiana na mada ambazo watapitia uliofanyika katika ukumbi wa MSD jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tawi la la TUGHE wa GCLA, Juvitus Mukela akitoa neno kwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA uliofanyika katika ukumbi wa msd jijini Dar es Salaam .
 Baadhi ya wajumbe katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa GCLA wakifuatilia mada kwenye mkutano huo.
  Picha za pamoja 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad